Obama | Habari za Ulimwengu | DW | 23.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Obama

Joseph Biden ameteuliwa kua makamo wa rais pindi Barack Obama akishinda uchaguzi wa rais November ijayo

Washington:


Mtetezi mteule wa kiti cha urais kutoka chama cha Democrat nchini Marekani,Barak Obama, amemteuwa senetor wa Delaware Joseph Biden kutetea wadhifa wa makamo wa rais.Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 65 ni mwenyekiti wa kamisheni ya masuala ya nchi za nje katika baraza la Senet las Marekani.Barack Obama ametangaza uamuzi huo mbele ya hadhara iliyokusanyika Springfield,katika jimbo lake la Illinois.Huko ndiko alikotangazia mwezi February mwaka jana,uamuzi wa kutaka kupigania wadhifa wa rais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Democrat.Mwanasiasa huyo anaesifiwa kwa kutopenda makubwa aligonga vichwa vya habari alipounga mkono uamuzi wa rais George W. Bush wa kuivamia Iraq mnamo mwaka 2003.

 • Tarehe 23.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F3Su
 • Tarehe 23.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F3Su
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com