Obama atua ghafula Baghdad,Irak | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Obama atua ghafula Baghdad,Irak

Akitoka Istanbul,Uturuki ,rais Obama alielekea baghdad na sio washington.

Obama (Baghdad)

Obama (Baghdad)

Rais Barack Hussein Obama, ameondoka leo adhuhuri nchini Uturuki kwa ziara isiotazamiwa ya kuvitembelea vikosi vya Marekani nchini Iraq. Bila ya kutazamiwa, ndege yake ya "AIRFORCE I" ilitua Baghdad,nchini Irak.

Rais Obama alipanda ndege "AIFORCE I" akiruka kutoka Istanbul baada ya ziara ya siku 2 nchini Uturuki,dola la kwanza kubwa la kiislamu kutembelewa na rais wa Marekani:Ziara ya rais Barack Obama ilioanza kwa matarajio makubwa, imemalizika kwa msangao makubwa:Bila kutazamiwa, ndege ya rais Obama "Aiforce I" ilioruka kutoka Istanbul,haikuelekea Washington bali Baghdad.

Hatua hii imefungua sifa mpya katika mkakati wa Rais Obama wa kuvikomesha kabisa vita visivyopendeza vya kujiingiza Iraq na kuelekeza uzito zaidi wa kijeshi nchini Afghanistan.Nchini Irak,Rais Obama amepangwa kukutana na majamadari wa Marekani na vikosi pamoja na kuzungumza na viongozi wa Iraq kwa njia ya simu.Anatumia mawasiliano ya simu kwavile hali mbaya ya hewa imemzuwia kutumia ndege ya helkopta kuonana nao binafsi.

Katika ziara yake ya siku 2 iliomalizika leo nchini Uturuki,rais Obama alionana na viongozi wa dini mbali mbali na kuhutubia wanafunzi.

Akichambua mbele yao sura ya Marekani angependa wawenayo,Rais Obama alisema huko Istanbul:

"Sisi ni nchi ya asili na jadi tofauti,makabila na dini mbali mbali ambazo zimekuja pamoja kwa maadili mamoja.Ni Mahala panapotoa fursa kwa kila mmoja ikiwa tu atajitahidi.Ikiwa usemi huo si kweli, mtu aitwae Barack Hussein Obama ,asingechaguliwa Rais wa Marekani.Hii ndio Amerika ningependa muijue."

Barack Obama in Afganistan

Obama akitembelea wanajeshi wa Marekani Afghanistan 2005

Wakosoaji wa Rais Obama katika ziara yake hii nzima inayoishia Irak, watadai kwamba, licha ya kutunga mkakati mpya wa kuendesha vita nchini Afghanistan,rais Obama ameshindwa kujipatia zaidi ya askari 5000 kutoka washirika wake wa NATO kuimarisha vikosi nchini Afghanistan.

Na ingawa ule mkutano wa kilele wa uchumi wa dola 20 tajiri mjini London uliafikiana kuchangia kitita cha Trilion moja kuustawisha uchumi,kupambana na pepo za wakwepaji kodi,Obama hakufaulu kuungwamkono mpango wake na Uingereza wa kuongezwa fedha zaidi na washirika kuutia jeki uchumi-hasa Ufaransa na ujerumani zilimzima hapo.

Wasaidizi wsa Rais Obama wana maoni mengine: Wanadai ziara yake ya kwanza imeanza kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni yake ya uchaguzi ya kustwisha ushirika wa Marekani na mataifa mengine uliochafuliwa n a mivutano katika sera za nje za utawala wa george Bush.Katika usuhuba mpyawa Marekani na ulimwengu wa kiislamu, Rais Obama alikutana na viongozi wa dini za kiislamu, kiyahudi,kikristu mjini Istanbul,Uturuki hii leo.

Akifuatana na maimamu 2 wakimuongoza katika msikiti maarufu wa karne ya 17 wa Sultanahmet Mosque au mashuhuri zaidi kwa jina la "msikitu bluu", Rais Barack hussei n Obama, alivua viatu kama ada za kiislamu zinavyotaka na kuingia msikitini humo pamoja na waziri-mkuu Tayyip Erdogan wa Uturuki katika hali ya ulinzi mkali.Pale alipooneshwa maandishi katika dari ya msikiti huo iliomtaja mjukuu wa mtume Muhammad Hussein,jina babu yake Barack au jina lake la kati, Rais Obama alitabasamu akionesha furaha-kwa muujibu wa shirika la habari la Anatolia.

Rais Obama alichanganya ziara yake katika msikiti huo kwa ziara nyengine katika Kanisa la zamani la karne ya sita "Hagia Sophia" ,lakini liligeuzwa msikiti pale ufalme wa Osmani ulipouteka mji wa Istanbul hapo 1453.Miaka ya 1930 likageuzwa makumbusho.

Rais Obama kabla kuondoka kwake alipendekeza kuchukuliwsa msimamo wa wastani kuelekea Israel, akidai dola hilo la kiyahudi sio chanzo za mabalaa yote katika Mashariki ya Kati.Kwani alidai kuna pande mbili katika kila suala.Obama lakini alitoa salamu kwa Israel,akiitaka kujali pia maslahi ya wapalestina.Rais Obama alikamilisha ziara yake hii kwa kuzuru ghafula leo Iraq.

Mwandishi:Ali,Ramadhan/AFPE Mhariri:M.Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com