OBAMA ATEULIWA RASMI.
28 Agosti 2008DENVER.
Seneta Barack Obama ameteuliwa rasmi kuwa mgombea urais wa chama cha demokratik.
Mgombea mwenzi katika wadhifa wa makamu wa rais Joseph Biden pia ameteuliwa rasmi.
Obama ni mwanasiasa wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kukiwakilisha chama cha demokratik katika kugombea urais nchini Marekani.
Aliteuliwa kwa kishindo kwenye mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika mjini Denver, Colorado.
Hapo awali katika hotuba ya kusisimua,aliekuwa mpinzani wake katika kuwania nafasi hiyo, seneta Hillary Clinton alitoa mwito kwa wafuasi wake wote wamwuunge mkono Barack Obama. Akihutubia wajumbe kwenye mkutano huo leo, naye aliekuwa rais wa Marekani bwana Bill Clinton ameahidi kufanya kila analoweza kumuunga mkono Barack Obama.
Bill Clinton amesema kuwa Obama yupo tayari kuwa rais wa Marekani.