Nyuma ya Pazia... | Mada zote | DW | 15.04.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Miaka 60 ya DW

Nyuma ya Pazia...

...wafanyakazi wengi wa DW hufanya kazi kwa saa 24 kutayarisha taarifa za habari, taarifa za uchambuzi, kurepoti kutoka maeneo ya matukio, mahojiano na taarifa simulizi kwa ajili ya radio, televisheni na mtandao.

''Unasikiliza Deutsche Welle''
......kwa mfano katika idhaa ya Kiamhara,mtangazaji wa kike Lidat Abebe akiwa mbele ya kipaza sauti akitangaza moja kwa moja kutoka kituo cha matangazo cha Bonn.Kiamhara ni miongoni mwa lugha 30 ambapo Deutche Welle huwasiliana na wasikilizaji, watamazaji na wale wenye kutumia mtandao.Idhaa hiyo hutowa habari moto moto kutoka Ujerumani na Ulaya halikadhalika repoti kuhusu na kutoka Ethiopia.Mpangillio unaweza kubadilika...
...kwa Deutsche Welle. Ni mada gani muhimu leo? Mtangazaji anaweza kuzungumza na maripota gani moja kwa kwa moja hewani? Habari gani kuu zinafunguwa matangazo yetu? Kwa idhaa nyingi kama vile idhaa ya Kirusi ya DW kila wakati ni wakati muhimu wa kusikilizwa na wasikilizaji wengi. Kwa sababu wakati Bonn na Berlin ni jioni Wladiwostok jua linachomoza tena.


Mtunzi wa vitabu Liao Yiwu akiwa katika mahojiano...
...na Matthias von Hein mkuu wa Idhaa ya Kichina. Deutsche Welle huwapa sauti watu wengi ambao katika nchi zao hawana uhuru wa kuzungumza au wana uhuru mdogo wa kuzungumza. Kusikilizwa kwa maoni tafauti ni kitu muhimu kwa vipindi vya Deutsche Welle kwa ajili ya watu ambapo nchini kwao uhuru wa vyombo vya habari unaminywa.Hayo mahojiano ni marefu mno...
...au katika repoti zitumike sehemu muhimu? Kishwar Mustafa wa Idhaa ya Kiurdu anashugulikia kanda ya sauti kwa kutumia kifaa cha digitali. Kwa hiyo anaweza kutayarisha repoti moja moja na kuwa tayari kurushwa hewani studioni.Elimu kama maarifa ya juu...
...huenezwa na mfululizo wa vipindi vya mchezo wa kuigiza 'Noa Bongo Jenga Maisha Yako' katika lugha sita zinazoweza kusikika kwa Afrika na tatu kwa bara la Asia. Vipindi hivyo kwa mfano vinasimulia vipi vijana wanajenga maisha yao au vipi wanaweza kujikinga na UKIMWI. Hadithi hizo hutungwa na watunzi vijana kutoka Afrika na Asia na huandaliwa na waigizaji hapa Pakistan.

Hakuna mapumziko...
...kwa Pia Castro, Carlos Delgado na wenzao. Kwani hivi sasa matangazo ya televisheni ya Kihispania kwa eneo la Amerika Kusini yanarushwa hewani kwa saa 24 kwa siku. Kwa jumla Deutsche Welle inarusha matangazo yake duniani kote kwa kupitia idhaa sita za Televisheni kwa lugha ya Kijerumani, Kigereza, Kihispania na Kiarabu.

Ni kipya,cha kisiasa na chenye mafanikio...
..."Mazungumzo ya Vijana " na kipindi kinachotangazwa kila wiki. Kipimdi hicho cha televisheni kina idadi kubwa ya watazamaji katika nchi za Kiarabu. Mtangazaji Jaafar Abdul Karim anajadili na wageni wake juu ya mambo yote ambayo huvutia vijana katika ulimwengu wote wa nchi za Kiarabu- kuhusu "Vugugu la Mapinduzi ya Machipuko katika Nchi za Kiarabu" na pia kuhusu maisha ya wageni nchini Ujerumani.Kila kitu kuhusu Ulaya...
... wakati Özelem Coskunanapoongoza kipindi hicho kinachoitwa "DW ile Avurupa" (Ulaya na DW) cha dakika 26. Tokea katikati mwa mwaka 2012 unaweza kuona kipindi hicho kwenye kituo cha serikali cha "TRT Uturuki". Vipindi kama hicho hutayarishwa pia na Deutsche Welle kwa ajili ya soko la televisheni nchini Poland Romania, Albania, Croatia, Bosnia, Macedonia na Bulgaria.

"Zimebaki sekunde 30 kabla ya kuanza kipindi..."
Mtangazaji anatakiwa awe makini studioni tayari kuwasilisha kwa watazamaji mada kuu ya siku, wakati wahariri na mafundi mitambo wanatakiwa kuhakikisha kipindi kinakwenda bila ya matatizo. Msimamizi wa vipindi huunganisha mahojiano na mhojiwa moja kwa moja hewani na anabadilisha ratiba ya vipindi kunapotokea habari muhimu.Kufafanuwa mfumo wa kutenganisha taka Ujerumani...
...kwa mwananchi wa Brazil. Kwa Nadia Pontes na Rafael Olivera ambao ni Wabrazil hiyo ni kazi ya kila siku. Huzifanyia marekebisho repoti za msingi, repoti kutoka maeneo ya matukio na mahojiano ili kwamba wananchi wa Brazil wanaotumia mtandao waweze pia kuzungumzia mada maalum za Kijerumani. Unaweza kusoma kwa kupitia mtandao habari za Deutsche Welle kwa lugha 30 kuanzia Kialbania, Kiswahli hadi Kituruki.


Msafara wa mtandao kupitia Mali...
...mwanablogi Boukary Konate ameuandaa ili kwamba wananchi wengi wa vijijini nchini mwake waweze kuingia kwenye matandao duniani kote. Katika blogu yake ya kutowa elimu "Fasokan" ameshinda Tuzo ya Bobs ya Deutsche Welle kwa mwaka 2012 katika fani maalum ya elimu na utamaduni. Tuzo hizo za Bobs zimekuwa zikitolewa na DW katika fani 17 tokea mwaka 2004 kwa kuzitunukia tovuti zilizotia fora.


Kujifunza uandishi wa kiwango bora...
...kwa mwaka waandishi vijana 20 hupatiwa Mafunzo ya Deutsche Welle kuambatana na muongozo wake, miongoni mwao ni Imtiaz Ahmad kutoka Pakistan. Hali ya aina yake kwa Mafunzo hayo ya Kimataifa ni kwamba ni kwa ajili ya waandishi vijana kutoka duniani kote. Ziada ya hilo Chuo cha Mafunzo ya Uandishi wa Habari cha 'Deutsche Welle Akademie' kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Bonn/Rhein-Sieg kinatowa shahada ya "Masomo ya Kimataifa ya Vombo vya Habari".Wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka duniani kote...
...wanaweza kuendeleza maarifa na ujuzi wao na chuo cha DW Akademie. Kwa mfano muongozo kuambatana na Mafunzo ya Kiangazi yanayotolewa Asia ya kati katika mji mkuu wa Kirgistan wa Bischkek kuhusu uandishi wa kisasa: Hapa washiriki wanajifunza kwa wiki 10 misingi ya maadili ya uandishi wa habari wa vyombo vya habari vya aina yote."Jojo anatafuta bahati ''...
...katika mafuzo yake mjini Köln. Wanafunzi wanaojifuza Kijerumani wanatoka kila nchi, wakati kijana huyo wa Brazil akijiandaa na mtihani ameweza kumudu shida za kuishi katika nyumba ya pamoja na wanafunzi wenzake na kufuzu. Sambamba na mafunzo yake anashiriki katika mfululizo wa kila wiki wa video ambapo watazamaji wanaweza kuwasiliana kwa kupitia mtandao wa Facebook na muigizaji wa kike.Michezo hiyo ya kuigiza ya video imetunukiwa mara nyingi. Jojo anashiriki tena na kuigiza na muigizaji wa kike wa tamthiliya Dorothea Kriegl.


Vyombo vya habari vinatimiza dhima gani...
...katika kuzuwiya mizozo, utekelezaji wa haki za binaadamu au katika sekta ya elimu? Masuala haya ni kitovu cha Jukwaa la "Vyombo vya Habari Duniani " linaloandaliwa kila mwaka na Deutsche Wellle mjini Bonn. Mara ya mwisho kulikuwa na washiriki zaidi 2,000 kutoka takriban nchi 100. Mada ya jukwaa la mwaka huu litakaloanza tarehe 17 hadi 19 Juni itahusu "Mustakabali wa Ukuaji wa Kiuchumi: Tathmini ya Vyombo vya Habari.


Mwandishi : Mohamed Dahman/DW
Mhariri : Hamidou,Oumilker