1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

NSU

Kundi la watu watatu linalojulikana kama "National Socialist Underground" liliwauwa watu tisa wenye asili ya kigeni nchini Ujerumani kati ya mwaka 2000 na 2009, na askari polisi wa kike.

Polisi ya Ujerumani na mashirika ya ujasusi yamekosolewa kwa kushindwa kubaini lengo la itikadi kali la mrengo wa kulia katika mauaji hayo, na kwa kutofuatia nyayo ambazo zingesaidia kukamatwa kwa kundi hilo. Kundi hilo lilibainika baada ya wawili kati ya waanchama wake, Uwe Mundlos na Uwe Böhnhardt, walipokutwa wamekufa katika gari linalotumiwa kama nyumba, kufuatia jaribio la wizi wa benki lililoshindwa. Wanaaminika kujiuwa baada ya kulichoma gari lao moto, inagwa mazingira hasa ya vifo vyao yanaendelea kuchunguzwa. Ukaguzi wa jengo walilojaribu kuchoma ulipelekea kugunduliwa kwa bastola ya askari polisi alieuawa. Mshirika wao mkuu aliebakia, Beate Zschaepe, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Huu ni mkusanyiko wa maudhui za DW kuhusu kundi la NSU.