Ni kilele cha miaka 50 ya DW Kiswahili | Masuala ya Jamii | DW | 22.02.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Ni kilele cha miaka 50 ya DW Kiswahili

Leo ni kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Idhaa ya Kiswahili ya DW. Maudhui ya sherehe hii inayofanikishwa kwa mdahalo mkubwa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania ni "Maarifa na Mwamko katika vyombo vya habari"

Workshop mit unseren Partnerstationen im Rahmen des 50-jährigen Bestehens unserer Redaktion (Kisuaheli). Copyright: DW/Mohammed Khelef

Kisuaheli Workshop mit Partnerstationen in Dar es Salaam Tanzania

Idhaa hii ya Kiswahili inaadhimisha miaka 50 ya uandishi wa habari uliotukuka kwa lugha ya Kiswahili. Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari za uhakika kwa lugha hiyo kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu.

Majadiliano kuhusu sekta ya habari.

The German Ambassador to Tanzania Klaus Peter Brandes addresses journalists during a Press Conference in Dar es Salaam on 20.02.2013 in preparation for the 50th Anniversary of DW Kiswahili. Copyright: DW/Mohammed Khelef

Waandishi wa habari na wawakilishi wa DW Kiswahili

Mdahalo unafanyika kuanzia saa 9 mchana kwa saa za Afrika Mashariki (22-02-2013 mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Mohamed Abulrahman maadhimisho hayo yanawakutanisha pamoja baadhi ya wachambuzi wanaoheshimika nchini Tanzania.

Aidha mesema hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt. Miongoni wa watakaofanikisha mjadala huo ni pamoja na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshimika nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo), Jenerali Ulimwengu (Mwandishi wa habari), Valerie Msoka (Mkurugenzi waTAMWA) na Maggid Mjengwa (Mtaalamu wa mitandao ya kijamii).

Fursa ya kubadilishana mawazo

Katika mdahalo huo wahudhuriaji watakuwa pia na fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na waandishi wa DW kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania.

Idhaa ya Kiswahili ya DW hutangaza mara tatu kwa siku kwa ajili ya maeneo ya Afrika ya Mashariki na Maziwa Makuu. Ikishirikiana na redio washirika. Sikikiliza mahojiano wa na Sudi Mnette akizungumza na Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Mohamed Abdulrahman, akiwa Dar es Salaam◄

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Josephat Charo

DW inapendekeza

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com