Neymar aadhibiwa katika Copa America | Michezo | DW | 20.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Neymar aadhibiwa katika Copa America

Nyota wa Brazil Neymar amepigwa marufuku ya mechi nne, maana kuwa hatoweza kucheza tena katika dimba la Kombe la Mataifa ya Amerika ya Kusini, japokuwa Brazil inaweza kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo.

Shirikisho la Kandanda la Amerika Kusini Conmebol limesema uamuzi huo ulikuja baada ya mshambuliaji huyo kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchuano wa Jumatano waliofungwa goli moja kwa bila na Colombia na “matukio yaliyofuata”. Shirikisho hilo pia limemtoza Neymar dola 10,000.

Hata ikiwa watasonga mbele katika dimba hilo hadi fainali, Brazil itakuwa na mechi nne tu zilizosalia maana kuwa Neymar atazikosa zote. Mshambuliaji wa Colombia Carlos Bacca, aliyehusika katika vurugu na Neymar amepigwa marufuku ya mechi mbili.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Abdu Mtullya