1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Bashir akubali kikosi mchanganyiko Dafur

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfx

Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amethibitisha kuunga mkono kwake kikosi cha mchanganyiko cha kulinda amani huko Dafur nchini Sudan kitakachoundwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika na wale wa Umoja wa Mataifa.

Katika baruwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayemalizia muda wake Kofi Annan Bashir pia amesema serikali yake iko tayari kutekeleza muafaka wa mpango wa amani.Mpango huo wa awamu tatu umerasimiwa baada ya serikali ya Sudan kuendelea kukataa uwekaji wowote ule wa kiwango kikubwa wa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa huko Dafur na kwamba kikosi mchanganyiko cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kiongozwe na kile cha Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo wanadiplomasia wanasema kwamba baruwa hiyo bado ingali ina vipengele vyenye utata.

Mzozo wa takriban miaka minne huko Dafur kati ya waasi na vikosi vya serikali pamoja na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali umegharimu maisha ya watu 200,000 na kuwapotezea makaazi wengine zaidi ya milioni mbili.