1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Neuer kusalia nahodha wa Bayern Munich

30 Julai 2018

Mabingwa wa soka wa Ujerumani Bayern Munich wamerudi nyumbani Jumatatu baada ya ziara yao ya kabla msimu kuanza huko Marekani.

https://p.dw.com/p/32KcO
FIFA Fußball-WM 2018 in Russland | Deutschland vs. Schweden
Picha: picture-alliance/dpa/Tass/V. Sharifulin

Ziara hiyo lakini haikuwaendea vyema Bayern baada ya kufungwa na Juventus katika mechi ya awali na mnamo Jumamosi Manchester City wakawafunga 3-2. Meritan Shabani aliwafungia Bayern bao la kwanza na Arjen Robben akafunga la pili huku Manchester City wakifungiwa na Bernado Silva aliyefunga mawili kisha Lukas Nmecha akafunga moja.

Ila matokeo hayo hayajawavunja moyo Bayern Munich kwa kuwa kocha wao mpya waliyemnunua kutoka Eintracht Frankfurt Niko Kovac amesema matayarisho yalikuwa mazuri licha ya kushindwa kwenye mechi mbili. Kovac amesema la muhimu kwake ni kwamba wachezaji wake wako imara. Wakati huo huo Kovac amesema Manuel Neuer ataendelea kuwa nahodha wa klabu hiyo akidai klabu hiyo in a wachezaji kadhaa walio na uwezo wa kuwa manahodha. Hii inamaanisha Thomas Müller ataendelea kuwa nahodha msaidizi.

Mwandishi: Jacob Safari/Reuters/DPA/AFP

Mhariri: Yusuf Saumu