Netanyahu apongeza kuokolewa kwa rubani wa Marekani
5 Aprili 2026
Katika hotuba iliyorekodiwa, Netanyahu amesema Waisraeli wote wanafurahia uokoaji huo wa ajabu wa rubani wa Marekani aliyemuita shujaa.
Ameongeza kusema operesheni hiyo ya uokoaji inatilia mkazo kanuni takatifu kwamba hakuna anayeachwa nyuma.
Katika hatua nyingine makundi ya kujihami yanayoiunga mkono Iran yamefanya mashambulizi mawili usiku wa kuamkia leo dhidi ya maeneo ya kidiplomasia ya Marekani nchini Iraq. Haya yamesemwa leo Jumapili na ubalozi wa Marekani nchini Baghdad.
Kwengineko mamlaka katika Umoja wa Falme za Kiarabu imeripoti uharibifu uliofanyika katika kiwanda cha petrokemikali cha Borouge, baada ya kuanguka kwa vifusi kutoka mifumo ya ulinzi wa anga.
Hakuna majeruhi walioripotiwa .
Mapema, mamlaka ilisema kuwa operesheni katika kiwanda hicho zilikatizwa kwasababu ya kuzuka kwa moto huo.