1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Nchi za kigeni ziko mbioni kuwaokoa raia wao Sudan

John Juma
24 Aprili 2023

Mzozo wa kivita unaoendelea Sudan umesababisha nchi kadhaa za kigeni kuwa mbioni kuwaondoa maafisa na raia wao nchini humo.

https://p.dw.com/p/4QV61
Sudan Khartum | Flucht Bewohner vor Kämpfen
Picha: EL TAYEB SIDDIG/REUTERS

Uwanja mkuu wa ndege mjini Khartoum umekuwa kitovu  cha mapigano makali na unadhibitiwa na kikosi chenye nguvu cha wanamgambo kinachofahamika kama Rapid Support Forces-RSF.

Kikosi cha RSF kinapambana dhidi ya jeshi.

Operesheni nyingi za uokoaji wa maafisa na raia zinafanywa kutoka bandari ya Sudan katika Bahari ya Shamu.

Miongoni mwa nchi ambazo zimefanikiwa kuondoa sehemu ya wananchi wao ni Marekani, Ujerumani, Saudi Arabia, na Canada huku nchi kadhaa pia zikiweka mikakati ya kuwaondoa raia wao.

Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa miungano na mataifa mengine ambayo yametaka mzozo huo kutatuliwa kwa haraka.