1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi za Afrika zahimizwa kushirikiana kukabili mihadarati

27 Juni 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa UNODC limesema vyombo vinavyosimamia sheria barani Afrika vinapaswa kushirikiana kwa karibu kukomesha biashara ya mihadarati aina ya Heroin na mingineyo

https://p.dw.com/p/30Pdi
Peru Zerstörung von Kokain durch die Polizei
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Mejia

Afisa wa ngazi ya juu katika ofisi ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu ya Umoja wa Mataifa UNODC amesema vyombo vinavyosimamia sheria barani Afrika vinapaswa kushirikiana kwa karibu kukomesha biashara ya madawa aina ya Heroin na mengineyo yanayoingizwa katika nchi zao.

Amando de Andres amesema serikali za barani Afrika zilikamata asilimia 1 tu ya tani 658 za bangi,tani 91 za heroin na tano 65 za madawa aina ya Mophine yaliyokamatwa duniani katika mwaka 2016.

Kwa mtazamo wa afisa huyo wa Umoja wa Mataifa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika hazijakamata kiasi kikubwa cha madawa hayo.

Katika ripoti ya mwaka 2018 kuhusu mihadarati duniani de Andre iliyozinduliwa Nairobi siku ya Jumatatu alisema kwamba hata nchi za Afrika ya Kati na Magharibi zimeshindwa kuchukua hatua kali.