1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi tajiri zahimizwa kupeleka chanjo za COVID-19 Afrika

9 Septemba 2021

Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika CDC John Nkengasong, ameyataka mataifa tajiri duniani kupeleka chanjo za Covid-19 barani Afrika kusaidia kupambana na janga la Covid19.

https://p.dw.com/p/407xk
John N. Nkengasong Afrika Africa Centres for Disease Control
Picha: Getty Images/M. Tewelde

Nkengasong amesema nchi tajiri zitakuwa zimefanya jambo la busara kwa kufanya hivyo badala ya kuzihodhi chanjo hizo kwa ajili ya kutoa chanjo za tatu za ziada kwa raia wao, jambo ambalo halijathibitishwa kisayansi.

Mkurugenzi huyo amesema ameshangazwa na jinsi baadhi ya nchi zinavyopuuza wito wa Shirika la Afya Duniani WHO wa kutotoa chanjo za tatu hadi pale idadi tosha ya watu watakapokuwa wamechanjwa kote duniani.

Kufikia sasa bara la Afrika limeandikisha maambukizi milioni 7.9 huku zaidi ya watu laki mbili wakiwa wamefariki dunia.