1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nchi 11 zinakutana nchini Gabon kujadili usalama

Sekione Kitojo
1 Desemba 2016

Kwa pamoja zimeutaka upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuunga mkono makubaliano yanayomruhusu Rais Joseph  Kabila kuendelea kubaki madarakani.

https://p.dw.com/p/2TZfB
Angola | Ankunft des kongolesischen Präsidenten Joseph Kabila bei einem meeting der süd- und zentralafrikanischen Staaten in Angola
Picha: REUTERS/K. Katombe

Nchi 11 zinazokutana kujadili usalama katika mataifa  ya Afrika ya kati, zimeutaka  upinzani  katika  Jamhuri  ya Kidemokrasi  ya  Congo kuunga mkono makubaliano yanayomruhusu Rais Joseph Kabila kuendelea kubaki madarakani baada ya muhula wake kumalizika.

Viongozi ama wawakilishi wao kutoka katika jumuiya ya kiuchumi  ya mataifa ya Afrika ya  kati  ECCAS , wanakutana  mjini  Libreville, mji  mkuu  wa  Gabon.

Kati ya mataifa  hayo 11 yanayoshiriki  katika mkutano huo uliofanyika  jana, manne yanawakilishwa na viongozi wakuu wa taifa, Rais Idriss  Derby Itno  wa Chad, Paul Kagame wa Rwanda, Faustin-Archange Touadera  wa Jamhuri ya Afrika ya kati na  mwenyekiti wa mkutano huo Ali  Bongo Ondimba wa Gabon.