1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Navalny kuzikwa Ijumaa

29 Februari 2024

Misa ya wafu ya kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny itafanyika Ijumaa katika kanisa moja mjini Moscow, wiki mbili baada ya kufariki akiwa jela.

https://p.dw.com/p/4d0EF
Hisia baada ya kifo cha Alexei Nawalny
Wafuasi wa Navalny wakibeba picha yake baada ya kifo chakePicha: Dawid Zuchowicz/Agencja Wyborcza.pl/REUTERS

Mjane wa Navalny, Yulia Navalnaya, anasema anahofia kwamba shughuli hiyo itatatizwa na kamatakamata.

Timu iliyokuwa inahusika na mazishi hayo imesema ilikuwa vigumu kupata kanisa lililokuwa tayari kufanya ibada ya wafu kwa ajili ya kiongozi huyo wa upinzani.

Ikulu ya Kremlin ilikuwa inahofia kwamba mazishi yoyote ya umma huenda yakageuka na kuwa maandamano ya kuonyesha uungaji mkono wa Navalny.

Mamlaka nchini Urusi zilikataa kuipa familia yake mwili kutokana na kile kilichosemekana kuwa ni jaribio la kuficha chanzo cha kifo chake.

Navalny atazikwa katika makaburi ya Borisov. rais Vladimir Putin hadi sasa amepiga kimya kuhusiana na kifo hicho cha mpinzani wake mkuu.