1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani atakua mrithi wa Johnson Uingereza?

21 Julai 2022

Wagombea wawili wanaowania nafasi ya waziri mkuu wa Uingereza wameanza harakati za kusaka kura za wanachama wa chama cha Conservative.

https://p.dw.com/p/4EUWe
Liz Truss und Rishi Sunak
Picha: picture alliance/PA Wire

Waziri wa zamani wa fedha Rishi Sunak, anaahidi busara ya kifedha, huku waziri wa mambo ya nje Liz Truss anaahidi kupunguza kodi mara moja kwa wanachama wa chama hicho tawala wa mrengo wa kulia.

soma Mpambano wa kuwania uongozi Uingereza waanza rasmi

Chama hicho kimegawanyika na kukosa ari baada ya miaka mitatu ya sokomoko chini ya utawala wa waziri mkuu anaeondoka Boris Johnson, ambaye alijiuzulu kama kiongozi wa chama Julai 7 baada ya miezi kadhaa ya kashfa za ukosefu wa maadili.

Hata hivyo Johson anasalia kuwa waziri mkuu hadi mrithi wake atakapochaguliwa na matokeo ya kinyang'anyiro cha uongozi wa chama yanatarajiwa tarehe 5 Septemba na mshindi moja kwa moja anakuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza.

soma Mbio za kumsaka waziri mkuu mpya wa Uingereza

Sunak na Truss walichaguliwa jana Jumatano na wabunge wa Conservative kama wagombea wa mwisho kutoka jumla ya wagombea 11 waliotangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.

Mchakato wa waziri mkuu mpya

Boris Johnson im UK Parlament
Bunge la UingerezaPicha: Jessica Taylor/UK Parliament/AP/picture alliance

Wanachama 180,000 wa Conservative ndiyo wana haki ya kumchagua kiogozi ajae wa taifa hilo, ambapo mshindi wa kinyang'anyiro cha sasa atakuwa waziri mkuu wa Uingereza hadi mwaka 2024, au iwapo atachagua kuitisha kura ya mapema.

Kura ya maoni inaashiria kwamba Truss ndiye chaguo la wengi na katika mahojiano alisema ana ushupavu na ujasiri wa kuongoza nchi katika nyakati za matatizo. Kwa upande wake Sunak anahoji kuwa itakuwa ni kutowajibika  iwapo watapunguza kodi kabla ya kudhibiti mfumuko wa bei.

Ushauri kwa atakayeshinda

Waziri Mkuu wa Uingereza anayeondoka Boris Johnson alishiriki katika kikao chake cha mwisho cha maswali kwa Waziri Mkuu bungeni jana na kusema:

"Nataka kutumia sekunde chache za mwisho Mheshimiwa Spika kutoa maneno ya ushauri kwa mrithi wangu, yeyote yule. Namba moja, kaa karibu na Wamarekani. Shikamana na Waukraine. Shikamana na Uhuru na demokrasia kila mahali. Punguza kodi na uondoe udhibiti popote uwezapo ili kufanya mahali hapa pawe pazuri pa kuishi na kuwekeza."

UK Fragen für den Premierministers | Boris Johnson
Picha: REUTERS

soma Kutoka Brexit hadi Partygate, hatimaye Johnson ajiuzulu

Kwa mujibu wa msemaji wa waziri mkuu anayeondoka, Boris Johnson anatarajiwa kuondoka ofisini Septemba 6, na atakwenda katika kasri la Buckingham kuwasilisha ombi la kujiuzulu kwa Malkia Elizabeth.