1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi wa Burundi ashitakiwa kwa kuhatarisha usalama

19 Aprili 2024

Mwandishi mmoja wa habari nchini Burundi ameshtakiwa kwa kosa la kuhatarisha usalama wa ndani, ambalo linamuweka katika hatari ya kukabiliwa na kifungo cha maisha jela.

https://p.dw.com/p/4ezGp
Burundi Evariste Ndayishimiye
Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.Picha: Tchandrou Nitanga/AFP/Getty Images

Sandra Muhoza, mwenye umri wa miaka 42, mwandishi habari wa gazeti la mtandaoni la La Nova Burundi alikamatwa na maafisa wa idara ya ujasusi ya Burundi mwishoni mwa juma lililopita katika mji mkuu. Bujumbura.

Soma zaidi: Burundi yaomba msaada kukabiliana na athari za mvua

Mawakili wake na jamaa zake wamedai kwamba mwandishi habari huyo alipigwa na maafisa wakati akihojiwa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.