1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanawe Michael Ballack afariki dunia katika ajali

6 Agosti 2021

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack anaomboleza kifo cha mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 18 Emilio, aliyefariki katika ajali mjini Lisbon, Ureno.

https://p.dw.com/p/3ybVd
Emilio Ballack | Sohn von Michael Ballack
Emilio Ballack, mwanawe Michael BallackPicha: Kerstin Dšlitzsch/Picture Point/imago images

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ujerumani Michael Ballack anaomboleza kifo cha mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 18 Emilio, aliyefariki katika ajali mjini Lisbon, Ureno.

Msemaji wa kitengo cha dharura katika hospitali ya Setubal nchini Ureno, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa Emilio amefariki dunia saa 2.17 alfajiri katika mji wa kitalii wa Troia, kusini mwa Lisbon.

Wazima moto na maafisa wa polisi walifika katika eneo la ajali ili kumsaidia lakini tayari Emilio alikuwa amefariki. Wanasaikolojia walikuwepo katika eneo la tukio ili kutoa msaada wa kisaikolojia kwa familia ya marehemu.

Ripoti za vyombo vya habari vya Ureno zimesema kuwa Emilio alikuwa akipeleka baiskeli yenye muundo mkubwa katika eneo la Troia, karibu na nyumba ya familia ya Ballack, wakati baiskeli yake ilipomuangukia.

Klabu ya Chelsea imeandika kwenye mtandao wao wa Twitter: " Kila mtu ndani ya klabu ameshtushwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Emilio Ballack. Mawazo yetu yote yako kwa babake Michael na familia yake kipindi hiki cha huzuni."

Emilio alizaliwa mwaka 2002. Ballack ambaye aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani pia amejaliwa watoto wengine wawili wa kiume, mmoja alizaliwa mwaka 2001 wakati mwengine alizaliwa mwaka 2005.