1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mwanariadha wa Kenya Kelvin Kiptum kuzikwa Februari 23

20 Februari 2024

Mwanariadha wa Kenya aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum atazikwa siku ya Ijumaa wiki hii katika kijiji chake cha Chapkorio huko Elgeyo Marakwet.

https://p.dw.com/p/4cdCb
Kiptum aaga dunia
Mwanariadha wa Kenya aliyeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum, kuzikwa Februari 23Picha: Eileen T. Meslar/Chicago Tribune/AP/dpa/picture alliance

Mwanariadha huyo na kocha wake raia wa Rwanda, Gervais Hakizimana walifariki dunia usiku wa Februari 11 katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la bonde la ufa karibu na nyumbani kwake huko Eldoret.

Kenya yaomboleza kifo cha mwanariadha Kelvin Kiptum

Kifo cha Kelvin Kuptum kiliwashtua wengi nchini Kenya na hata kimataifa hasa ikiwa ni miezi michache tu kabla ya kuanza kwa Michezo ya Olimpiki ya ya mjini Paris.