Mvutano kati ya Hamilton na Rosberg wapamba moto | Michezo | DW | 26.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mvutano kati ya Hamilton na Rosberg wapamba moto

Timu ya Mercedes imesajili ushindi wake wa sita mfululizo msimu huu katika mbio za magari ya Formula One, baada ya kutawala mkondo wa Monaco Grand Prix, Ufaransa.

Lakini mvutano unaoendelea kuongezeka baina ya madereva wawili, Lewis Hamilton na Nico Rosberg una maana kuwa timu hiyo ina sababu ya kuwa na wasiwasi. Mkondo wa Canadian Grand Prix ndio unaofuata lakini kabla ya mataa kugeuka na kuwa ya kijani mjini Montreal Juni 8, wakuu wa Mercedes watakuwa na hamu ya kuhakikisha kuwa mahusiano baina ya madereva hao wawili yanaimarika.

Ushindi wa Nico Rosberg katika mkondo wa Monaco umemsongeza points nne mbele ya Hamilton kileleni mwa msimamo wa ubingwa wa madereva lakini ulipatikana katika mazingira yenye utata ambayo bila shaka yalimkasirisha dereva mwenza Hamilton.

Nico Rosberg ana ufahamu mzuri wa barabara za Monaco kuwaliko madereva wengine

Dereva wa Mercedes Nico Rosberg ana ufahamu mzuri wa barabara za Monaco kuwaliko madereva wengine

Wakati muda ukiyoyoma katika mashindano ya kufuzu siku ya Jumamosi, Rosberg alipoteza mwelekeo kwenye kona na kisha kwa kulirudisha gari lake nyuma kurejea kwenye mkondo sahihi luhakikisha kuwa Hamilton hangeweza kumaliza kwa kasi mzunguko wa mwisho katika juhudi za kumaliza mbele ya Roseberg.

Baada ya uchunguzi, Rosberg hakupatikana na makosa na hivyo ikamaanisha kuwa angeanza katika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Jumapili ya Monte Carlo, Monaco. Lakini ni kama hatua hiyo imemfanya Hamilton kushindwa kusaheme na kusahau.

Alipoulizwa kama yeye na Rosberg watazungumzia hali hiyo ili kurejesha utulivu, Hamilton alijibu “kwa kweli sina jibu kuhusu hilo”. Naye Rosberg alijibu suali hilo akisema “tumekuwa na mazugnumzo na uzuri ni kwamba tumefahamiana kwa muda mrefu. Sisi hukaa na kuzungumza na kisha kusongambele, na hilo ndio tunalifanya wikendi hii”.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu