Musk akosa kufika Paris kwa uchunguzi kuhusu mtandao wa X
20 Aprili 2026
Waendesha mashtaka wameiambia AFP wamezingatia kutokuwepo kwa watu wa kwanza walioitwa,bila kutaja moja kwa moja jina la Musk.
Musk alitakiwa kutoa maelezo katika tukio ambalo wachunguzi wanachunguza madai ya utovu wa nidhamu unaohusishwa na mtandao wa kijamii wa X, hii ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa nyenzo za unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na maudhui kwenye mtandao unaotumia teknolojia ya akili mnemba, Deepfake.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Paris, imesema Musk pamoja na mkuu wa zamani wa X Linda Yaccarino, walitakiwa kufika kwa mahojiano ya hiari huku wafanyakazi wengine wa mtandao huo wakitarajiwa kutoa ushahidi wao wiki nzima.
Msemaji wa X hakujibu maswali kutoka kwa shirika la habari la AP na kampuni ya sasa ya Yaccarino, eMed, pia haikujibu ombi la tamko kuhusu tukio hilo.