Mubarak ajiuzulu
11 Februari 2011Matangazo
Rais Mohamed Hosni Mubarak wa Misri hatimae amejiuzulu hatua inayomaliza miaka 30 ya utawala wake wa kimabavu. Mubaraka melikabidhi madaraka baraza la uongozi wa majeshi ya nchi hiyo. Tangazo la kujiuzulu kwake limetolewa na Jenerali Omar Suleiman alimteuwa hivi karibuni kuwa makamu wake wa rais. Hapo kabla iliripotiwa kwamba Mubarak na familia yake wameondoka kwa ndege ya kijeshi mjini Cairo na kwenda katika mji wa kitalii wa Sharm el-Sheikh. Kwa sasa ni mapema kufahamika iwapo atabakia Misri au ameondoka.