1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Aliyemshambulia mume wa Nancy Pelosi ahukumiwa miaka 30 jela

18 Mei 2024

Mahakama nchini Marekani imemhukumu miaka 30 jela mwanaume mmoja aliyemshambulia kwa nyundo mume wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi.

https://p.dw.com/p/4g1NK
Nancy Pelosi (kushoto) akiwa na mumewe Paul Pelosi.
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi (kushoto) akiwa na mumewe Paul Pelosi.Picha: Fabio Frustaci/ANS/ZUMA//picture alliance

David DePape alipatikana na hatia mwaka jana kwa kuingia kinyume cha sheria kwenye nyumba ya wanandoa hao mjini San Francisco na kumshambulia  Paul Pelosi katika shambulio la kutisha lililonaswa na kamera za usalama.

Tukio hilo lilifanyika mnamo mwezi Oktoba mwaka 2022.

Awali, waendesha mashtaka walikuwa wameiomba mahakama ya shirikisho huko San Francisco kumhukumu DePape kifungo cha miaka 40 jela. Watu wengine ambao mshtakiwa huyo alikiri kutaka kuwashambulia ni pamoja na Gavana wa California Gavin Newsom, mtoto wa Rais Joe Biden - Hunter, na mwigizaji Tom Hanks.