1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msumbiji yakabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa kipindupindu

31 Machi 2023

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema Msumbiji inakabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa kipindupindu katika kipindi cha mwongo mmoja, kutokana na kimbunga Freddy kilichoipiga nchi hiyo

https://p.dw.com/p/4PZDz
Afrika Mosambik Cholera
Picha: Marcelino Mueia/DW

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema Msumbiji inakabiliwa na mripuko mbaya zaidi wa kipindupindu katika kipindi cha mwongo mmoja, kutokana na kimbunga Freddy kilichoipiga nchi hiyo.

Soma pia: Waliokufa kwa kimbunga Malawi na Msumbiji wapindukia 200

Mwakilishi wa WHO katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika, Severin von Xylander, amesema ingawa Msumbiji hushuhudia mripuko wa kipindupindu kati ya Oktoba na Aprili huku kukiripotiwa karibu visa 21,000 na vifo 95, mripuko huu wa sasa ndio mkubwa zaidi.

Von Xylander amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba mripuko huo unazidi kuenea ambapo mikoa minane kati ya 11 ya nchi hiyo imeathirika.

Kimbunga Freddy kiliharibu zaidi ya makaazi 130,000 na kuwaacha watu 184,000 bila makao na ingawa mafuriko yanapungua kwa sasa, kupata maji safi ni changamoto.