1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Msimu wa Kimpembe wafikia mwisho baada ya jeraha

27 Februari 2023

Msimu wa beki wa PSG, Presnel Kimpembe umemalizika mapema baada ya beki huyo wa kati kupata jereha litakalompelekea kufanyiwa upasuaji katika ushindi wao wa 3-0 Jumapili walipokuwa wakicheza na Olympique Marseille.

https://p.dw.com/p/4O1vH
EURO 2020 | Frankreich vs Schweiz | Tor Gavranovic
Picha: Marko Djurica/REUTERS

Kimpembe ambaye alikosa kushiriki Kombe la Dunia huko Qatar kutokana na jeraha aliondolewa uwanjani kunako kipindi cha kwanza, hiyo ikiwa ni wiki mbili tu baada ya kurudi uwanjani kutoka kwenye jeraha lililomuweka nje kwa miezi mitatu.

Ushindi wa jana ambapo Kylian Mbappe na Lionel Messi walitikisa wavu, umewapelekea PSG kuwa pointi nane kileleni kabla kucheza na Nantes Jumamosi ijayo aktika mpambano wa ligi.