1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa aliyempiga risasi Robert Fico afikishwa Mahakamani

18 Mei 2024

Mshukiwa aliyeshitakiwa kwa jaribio la kumuua Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico amewasili katika mahakama itakayoamua kuhusu kuzuiliwa kwake kabla ya kusikilizwa kwa kesi yake.

https://p.dw.com/p/4g1gf
Slovakia |Handlova
Polisi ya Slovakia ikimkamata mshukiwa aliyempiga risasi Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico Picha: Radovan Stoklasa/AP Photo/picture alliance

Mwanamume huyo aliyetambuliwa na vyombo vya habari vya Slovakia kama poet Juraj Cintula, aliye na miaka 71 alimpiga risasi mara nne Fico muda mfupi baada ya kuongoza kikao cha baraza la mawaziri mjini Handlova siku ya Jumatano wiki hii. Waziri Mkuu huyo alikuwa akielekea upande wa wafuasi wake wakati tukio hilo lilipotokea. 

Fico aliyejeruhiwa tumboni, alikimbizwa hospitalini ambako hadi sasa amefanyiwa upasuaji mara mbili lakini bado maafisa nchini Slovakia wanasema hali yake sio ya kuridhisha.

Waziri Mkuu wa Slovakia amepigwa risasi na kujeruhiwa

Slovakia yenye wakazi milioni 5.4 na ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya, haina historia pana ya vurugu za kisiasa na tukio hilo limeushtua ulimwengu huku viongozi mbalimbali wakilaani kisa hicho akiwemo kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.