Msalaba Mwekundu wasitisha huduma Sudan Kusini | Matukio ya Afrika | DW | 15.09.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

SUDAN KUSINI

Msalaba Mwekundu wasitisha huduma Sudan Kusini

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) limesema kuwa limesitisha shughuli zake katika eneo linalokumbwa na vita Sudan Kusini baada ya mfanyakazi wake mmoja kuuawa wiki iliyopita wakati akipeleka misaada.

Msemaji wa ICRC, Mari Aftret Mertvert, amesema kwa sasa shughuli zao zimesimama katika mkoa wa Equatoria na kwamba wanajaribu kuchunguza kilichotokea.

Dereva wa shirika hilo aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wenye silaha wakati akiendesha msafara wa malori ya misaada katika mkoa huo ulioko magharibi mwa Sudan Kusini.

Maelfu ya watu wameuawa na wengine milioni 3.8 wameyakimbia makaazi yao kutokana mzozo unaoendelea nchini humo.

Kwa mujibu wa ofisi inayoshughulika na misaada ya kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya wafanyakazi 80 wa mashirika ya kutoa misaada wameuawa Sudan Kusini tangu Desemba 2013.