1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mourinho apigwa kalamu Tottenham Hotspur

Admin.WagnerD19 Aprili 2021

Jose Mourinho amepigwa kalamu kama kocha wa Tottenham Hotspur siku sita tu kabla ya kucheza fainali ya Kombe la Ligi maarufu kama Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City. Ni baada ya matokeo ya kutoridhisha

https://p.dw.com/p/3sEnf
UEFA Champions League | Tottenham Hotspur v RB Leipzig | Jose Mourinho
Picha: Imago Images/Picture Point LE

Jose Mourinho amepigwa kalamu kama kocha wa Tottenham Hotspur siku sita tu kabla ya kucheza fainali ya Kombe la Ligi maarufu kama Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City.

Taarifa ya Spurs imethibitisha kuwa Mreno huyo ameondoka pamoja na kikosi cha benchi la kiufundi. Kocha huyo wa zamani wa Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid na Manchester United alijiunga na Spurs Novemba 2019 akichukua nafasi ya Mauricio Pochettino. Matumaini ya klabu hiyo kumaliza katika nne bora yalifutwa na sare ya 2 -2 dhidi ya Everton.

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy, aliyemuajiri Mourinho kwa sababu ya ujuzi wake wa kushinda mataji, amesema mambo hayakwenda kama walivyotarajia. Kiungo wa zamani Ryan Mason atashikilia usukani wa kikosi cha kwanza hadi mwisho wa msimu.

AFP/DPA/AP/Reuters