Moto wauwa watu 40. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Moto wauwa watu 40.

Abuja. Nchini Nigeria kiasi watu 40 wameuwawa katika moto ambao umezuka baada ya bomba la mafuta kuharibiwa karibu na mji wa Lagos. Watu kadha ambao walikuwa wakijaribu kuchota mafuta kutokana na kutoboka kwa bomba hilo walizingirwa na moto. Maafisa wa shirika la msalaba mwekundi katika eneo hilo wamesema kuwa wahanga wengi walikuwa wanawake na watoto. Uharibifu mara nyingi hutokea katika mabomba ya mafuta nchini Nigeria ili kuiba mafuta ambayo huuzwa kwa magendo. Mamia ya watu wamekufa wakichota mafuta kutoka katika mabomba yaliyopasuka nchini Nigeria katika miezi ya karibuni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com