Moscow. Wachimba migodi 78 wauwawa.
20 Machi 2007Matangazo
Maafisa nchini Russia wamethibitisha vifo vya kiasi watu 78 wachimba migodi kutokana na mlipuko wa gesi katika eneo la machimbo ya mkaa wa mawe katika jimbo la kati la Siberia.
Vikundi vya kutoa msaada wa dharura hadi sasa vimewaokoa zaidi ya watu 80 , lakini wengine kadha wanaripotiwa kuwa hawajulikani waliko na operesheni ya uokozi inaendelea.
Karibu wachimba migodi 200 walikuwa chini ya ardhi wakati mlipuko huo ulipotokea katika eneo la Kemerovo katika jimbo la Siberia. Sababu ya mlipuko huo bado inachunguzwa.