Mogadishu. Mapigano makali yazuka. | Habari za Ulimwengu | DW | 22.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mogadishu. Mapigano makali yazuka.

Nchini Somalia kiasi watu 14 wameuwawa katika mapigano makali kati ya wapiganaji wa Kiislamu na majeshi ya Ethiopia katikati ya mji wa Mogadishu.

Mapigano hayo yalianza karibu na kituo cha serikali katika yaliyokuwa makao makuu ya zamani ya wizara ya ulinzi, ambapo wapiganaji wamekuwa mara kwa mara wakishambulia wanajeshi wa jeshi la serikali na lile la Ethiopia walioko hapo.

Watu walioshuhudia wamesema wapiganaji hao walichoma na kuiburuza miili ya wanajeshi waliouwawa katika mitaa.

Serikali ya mpito ya Somalia ikiungwa mkono na majeshi ya Ethiopia iliuchukua mji wa Mogadishu kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu Desemba mwaka jana.

Umoja wa Afrika unapanga kutuma wanajeshi 8,000 wa kulinda amani kulisaidia jeshi la serikali kuchukua udhibiti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com