MOGADISHU : Mapigano makali yazuka mjini Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU : Mapigano makali yazuka mjini Mogadishu

Mapigano makali ya mizinga mjini Mogadishu yameuwa zaidi ya watu 10 leo hii.

Mapigano hayo yalikuwa sehemu ya mapambano makali katika mji mkuu wa Mogadishu tokea serikali ikisaidiwa na vikosi vya Ethiopia kuuteka mji huo kutoka kwa viongozi wa muungano wa mahkama za Kiislam mwishoni mwa mwaka jana.

Wanajeshi wa Somalia na Ethiopia wameshambuliwa vikali leo asubuhi na wamejibu mashambulizi hayo kwa mizinga katika sehemu mbali mbali za mji mkuu huo.

Madarzeni ya wananchi wa Somalia wameuwawa katika mashambulizi mwaka huu.Umoja wa Afrika unapanga kupeleka wanajeshi wa kulinda amani kuchukuwa nafasi ya wanajeshi wa Ethiopia ambao wameanza kuondoka nchini Somalia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com