Moenchengladbach wakwea kileleni Bundesliga | Michezo | DW | 07.10.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Moenchengladbach wakwea kileleni Bundesliga

Msimu huu wa Bundesliga unaonekana kuwa wenye kusisimua zaidi ukilinganishwa na misimu iliyopita. Kwa sasa jumla ya timu saba kutoka kileleni zimepishana kwa pointi mbili tu baina yao.

Hali hii imesababishwa na kushindwa mbili moja kwa Bayern Munich mnamo wikendi walipocheza nyumbani kwao Allianz Arena dhidi ya Hoffeheim na pia Borussia Dortmund kutoka sare ya magoli mawili na Freiburg nao RB Leipzig kutoshana nguvu na Bayer Leverkusen kwa bao moja kwa moja.

Sasa Borussia Moenchengladbach ndio waliokwea hadi kileleni mwa jedwali la Bundesliga. Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Moenchengladbach kuongoza ligi hiyo tangu msimu wa mwaka 2011/12.

Timu nyengine ambayo inaonekana kuwashangaza wengi na matokeo yake msimu huu ni VfL Wolfsburg ambayo kufikia sasa ndiyo timu ya pekee kwenye Bundesliga ambayo haijafungwa na kwa sasa wanaishikilia nafasi ya pili.

DW inapendekeza