Mlipuko watokea jijini Nairobi
11 Juni 2007Matangazo
Chanzo cha mlipuko bado hakijajulikana ila kwa mujibu wa Kamishna wa polisi Mohamed Hussein Ali mlipuko ulisababishwa na kitu kilichobebwa na mtu.
Polisi wanaeleza kuwa uchunguzi wa kwanza unabaini kuwa mtu mmoja alijaribu kuingia mkahawa mmoja nao walinzi walijaribu kumzuia kuingia kwani alikuwa na mavazi ya kutatanisha. Haijulikani iwapo mtu huyo alihusika na mlipuko huo.Mlipuko huo umetokea kwenye duka moja katika Hoteli ya Ambassadeur. Hoteli yenyewe haikuathirika.