1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa Wagner asema wapiganaji wake wameingia Urusi

24 Juni 2023

Kiongozi wa kundi la mamluki wa Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin, amesema leo kuwa wapiganaji wake wamevuka mpaka kutoka Ukraine kuingia Urusi na wako tayari kuchukuwa hatua zozote dhidi ya jeshi la Urusi.

https://p.dw.com/p/4T0hw
Russland | Prigoschin Videoansprachen in Rostow am Don
Picha: Prigozhin Press Service/AP Photo/picture alliance

Katika rekodi ya sauti kupitia mtandao wa Telegram, Prigozhin amesema kuwa wapiganaji wa Wagner walikuwa wameingia katika mji wa Kusini wa Urusi wa Rostov na kwamba yeye na wapiganaji wake, watakabiliana na yeyote atakayeleta upinzani.

Soma zaidi: Mkuu wa Wagner asema jeshi la Urusi linamdanganya Rais Putin

Mapema Ijumaa, Urusi ilimshutumu Prigozhin kwa kutoa wito wa uasi wa kijeshi baada ya kudai bila ya kutoa ushahidi kwamba uongozi wa jeshi la Urusi ulisababisha vifo vya idadi kubwa ya wapiganaji wake katika shambulio la anga na kuapa kuuadhibu.

Prigozhin amesema kuwa kambi za kundi hilo la Wagner zilishambuliwa kwa roketi na mizinga kwa amri kutoka kwa mkuu wa Utumishi wa Jeshi Valery Gerasimov. Prigozhin ameongeza kuwa Gerasimov alitoa agizo hilo baada ya mkutano na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu, ambapo waliamua kuliangamiza kundi hilo la Wagner