1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Mkuu wa Wagner asema jeshi la Urusi linamdanganya Putin

22 Juni 2023

Kiongozi wa kundi la mamluki wa Urusi la Wagner Yevegeny Prigozin ameushutumu uongozi wa jeshi la Urusi kwa kumdanganya Rais Vladimir Putin na kuficha ukweli juu ya hali ilivyo katika uwanja wa vita nchini Ukraine

https://p.dw.com/p/4Swz9
Wagner Gruppe Yevgeny Prigozhin / Jewgeni Wiktorowitsch Prigoschin
Picha: Lev Borodin/TASS/dpa/picture alliance

Kiongozi wa kundi la mamluki wa Urusi la Wagner Yevegeny Prigozin ameushutumu uongozi wa jeshi la Urusi kwa kumdanganya Rais Vladimir Putin na kuficha ukweli juu ya hali ilivyo katika uwanja wa vita nchini Ukraine.

Soma pia: Urusi yadai kuzima mashambulizi mengine ya Ukraine

Amesema kupitia ukurasa wa Telegram kwamba, Ukraine tayari imefanikiwa pakubwa na kuna maeneo makubwa yambayo wameyapoteza, na kwa mara nyingine akiwatupia lawama Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa Utumishi wa Jeshi Valery Gerasimov kwa kumdanganya Rais Vladimir Putin.

Prighozin amesema Urusi imepata hasara kubwa na matatizo sugu na endelevu yamekuwa yakifichwa.

Amesema, kwa upande mwingine uongozi wa jeshi la Urusi umekuwa ukiripoti uharibifu mkubwa wa mifumo ya teknolojia ya upande wa Ukraine lakini bila ya kutoa ushahidi wowote.