Mkurugenzi wa michezo BvB, Zorc asifu maendeleo ya FC Bayern | Michezo | DW | 27.09.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Mkurugenzi wa michezo BvB, Zorc asifu maendeleo ya FC Bayern

Kabla ya pambano lao katika  Super Cup dhidi  ya  Bayern Munich siku  ya  Jumatano, mkurugenzi  wa  spoti wa  Borussia Dortmund Michael Zorc  meisifu Bayern kama mfano wa kufuatwa.

"Msimu  uliopita  kikosi  cha  Bayern  chini  ya  uongozi  wa  Hansi Flick, tulishuhudia  utayari maalum  wa  kutoa  asilimia  100  uwanjani  kwa  kila  hali," Zorc aliliambia  gazeti  la  Jumapili  la  frankfurter Allgemeine.

"Na  bila shaka , tunataka nasi pia  kuelekea katika  mwelekeo  huo," alisema.

Michael Zorc Sportdirektor von Borussia Dortmund

Mkurugenzi wa spoti wa BvB Michael Zorc

Kwa upande wa Jadon Sancho  na  Jude Bellingham , Dortmund  imeongeza  chipukizi mwingine  kutoka  Uingereza  kwa  kumpa kandarasi  Jamie Bynoe-Gittens, mwenye  umri wa  miaka  16, ambae  aliwasili  wiki  iliyopita kutoka  Manchester City. Lakini  Zorc  alisema anafuraha  kwamba  kikosi  chake  kina mchanganyiko wa  vijana chikukizi na  wenye uzoefu.

"Hususan ni muhimu  kama  alivyosainiwa  Jude Bellingham pia  ni  muhimu  kwa  Thomas Meunier , ambaye  anakuja  na  uzoefu mkubwa  alionao, mtazamo wa  hali  ya juu  pamoja na nguvu alizonazo," alisema  kuhusiana  na  mchezaji  huyo  mpya  kutoka Paris Saint-Germain.

Pokalfeier Borussia Dortmund

Michael Zorc(kushoto) akishikilia kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal

Na Zorc alimkingia  kifua  kocha  wa  Borussia  Dortmund  ambaye  mara  kwa  mara hukosolewa. "Nilisema msimu mzima uliopita  kwamba  hapa  Dortmund hatujadili  nafasi ya kocha , lakini inaelekea  hakuna  mtu  anayetaka  kusikia  hilo," alisema. "Sihusiki  na  uvumi na minong'ono , na kwa ukweli  kabisa, sina nia  ya  kushughulikia  suala  hilo pamoja nao."