1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mjerumani Tuchel kukinoa kikosi cha England mwakani

Sylvia Mwehozi
17 Oktoba 2024

Thomas Tuchel ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya kandanda ya England, huku Chama cha Soka nchini humo FA kikimgeukia Mjerumani huyo kujaribu kutwaa taji lao la kwanza tangu mwaka 1966

https://p.dw.com/p/4ltGP
Kocha Thomas Tuchel
Kocha Thomas Tuchel Picha: Matthias Schrader/AP/picture alliance

ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya kandanda ya England, huku Chama cha Soka nchini humo FA kikimgeukia Mjerumani huyo kujaribu kutwaa taji lao la kwanza tangu mwaka 1966. Tuchel ambaye amewahi kuwa meneja wa klabu ya Chelsea ataanza kibarua chake Januari mosi mwakani. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51, ambaye amekuwa kando tangu aagane na Bayern Munich mwishoni mwa msimu uliopita, anarithi mikoba ya Muingereza Gareth Southgate kama kocha wa kudumu.

Anakuwa meneja wa tatu wa kigeni wa England baada ya Sven-Goran Eriksson na Fabio Capello. Tuchel, ambaye pia amezifundisha Borussia Dortmund na Paris Saint-Germain, anapewa matumaini ya kumaliza ukame wa miaka 58 wa England kushinda mashindano makubwa tangu Kombe la Dunia la 1966 kwenye ardhi ya nyumbani.