Misri yamzika Hosni Mubarak kwa heshima za kijeshi | Matukio ya Afrika | DW | 26.02.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Misri yamzika Hosni Mubarak kwa heshima za kijeshi

Misri inafanya mazishi ya heshima za kijeshi, ya aliyekuwa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani wakati wa wimbi la vuguvugu la maandamano.

Misri inafanya mazishi ya heshima za kijeshi, ya aliyekuwa rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani wakati wa wimbi la vuguvugu la maandamano ya umma katika ulimwengu wa Kiarabu. Mubarak, ambaye aliitawala Misri kwa miongo mitatu, alifariki dunia jana katika hospitali moja ya mjini Cairo akiwa na umri wa miaka 91. Televisheni ya taifa imesema maafisa wa ngazi ya juu wamealikwa kuhudhuria mazishi hayo ya kijeshi, bila kutoa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, Mubarak atazikwa katika eneo la makaburi ya familia mjini Cairo. Kiongozi huyo wa zamani na wanawe wawili walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani na kutakiwa kulipa faini ya mamilioni ya dola kwa ubadhirifu wa pesa za serikali. Mubarak alitumikia muda mwingi wa kifungo chake hicho hospitalini, na hatimaye kuachiliwa huru mnamo mwkaa 2017.