Milango ya msimu mpya wa Bundesliga yafunguliwa | Michezo | DW | 22.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Milango ya msimu mpya wa Bundesliga yafunguliwa

Msimu mpya wa Bundesliga umeng'oa nanga. Lakini mafanikio ya Ujerumani katika Kombe la Dunia yana maana gani katika kandanda la Bundesliga? Jee, Bundesliga iko tayari kumenyana tena kimataifa?

Mafanikio ya timu ya taifa ya Ujerumani nchini Brazil yameipiga jeki ligi ya Ujerumani ambayo tayari inaendelea kunawiri na hata kujipiga kifua kutokana na idadi kubwa zaidi ya mashabiki wanaohudhuria mechi viwanjani barani Ulaya.

Ujerumani badi ni ya tatu nyuma ya Uhispania na England katika msimamo wa viwango vya UEFA na pia iko nyuma ya Premier League katika mapato yanayotokana na shughuli za mauzo.

Lakini Bundesliga inaamini kuwa imepata mafanikio mazuri kuliko mahasimu wake wa Ulaya na sasa iko katika hali nzuri. Inajivunia tikiti za bei nafuu kuanganlia viwanjani, usimamizi mzuri wa kifedha, sheria kuhusu umiliki wa vilabu na aina ya uwekezani katika mafunzo ya soka la vijana ambao ulizaa matunda katika Kombe la Dunia nchini Brazil.

Fussball FC Bayern gegen Borussia Dortmund

Miamba wa Bundesliga Bayern na Dortmund wanatarajiwa kuwa na ushindani mkali msimu huu

Bayern inapigiwa upatu kutwaa taji la tatu la Bundesliga mfululizo lakini ni wzai kuwa mara hii itakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa hasimu wake mkuu Borussia Dortmund. Na huku kikosi chake kikionekana kuyumbayumba kwa sasa, Pep Guardiola amekiri kuwa atakuwa na wakati mgumu wakati wa kuanza kampeni yao

Usimamizi wa Dortmund umetangaza kuwa utauza hisa karibu milioni 24.5 kwa kiasi cha hadi euro milioni 114.4 ambapo baadhi ya fedha hizo zitatumika katika kulipia madeni ya klabu hiyo. Huyu hapa Meneja mkurugenzi wa Dortmund Hans-Joachim Watzke "Borussia Dortmund huenda hivi karibuni haitakuwa na madeni yoyote na hivyo itaweza kuwa na raslimali za kutosha lakini hatutapoteza ukarimu wetu, tutaendeleza malengo yetu na uhalali wetu. Kwa wale ambao huenda wakahofia kuwa filosofia yetu au sera huenda zikabadilika kwa kuwajumuisha wadau wapya, nasema kwamba pande zote tatu zinazohusika zimesisitiza kuwa maamuzi yote ya utendaji yatafanywa na usimamizi kama kawaida".

Bayer Leverkusen na Schalke 04 pia zimejiimarisha kwa ajili ya kusababisha ushindani mkali kileleni mwa ligi. Hivyo ni nani atakayeshinda taji la mwaka huu?

Mwandishi: Bruce AMANI/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu