Michuano ya Kombe la DFB Pokal kuendelea | Michezo | DW | 19.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michuano ya Kombe la DFB Pokal kuendelea

Bayern Munich inafukuzia fursa ya kukamata vikombe vitatu kama ilivyofanya mwaka 2013 wakati walioongeza ubingwa wa Bundesliga na vikombe katika mataji yao ya Ulaya

Bayern Inapambana na Bremen , inayopambana kujinasua kutoka kutumbukia katika ligi daraja la pili msimu ujao, uwanjani Allianz Arena ili kupata nafasi ya kushiriki katika fainali ya kombe la shirikisho DFB Pokal hapo Mei 21 katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin.

Borussia Dortmund itakuwa ugenini ikikaribishwa na Hertha Berlin katika nusu fainali nyingine hapo Jumatano.

Baada ya kuaga michuano ya Europa League katika robo fainali, Borussia inataka kufikia fainali ya mwaka huu ya kombe la Ujerumani baada ya kupoteza fainali ya mwaka 2015 dhidi ya Wolfsburg kwa mabao 3-1.

Hertha iliangukia pua dhidi ya Hoffenheim kwa mabao 2-1 katika ligi Jumamosi, ikiwa si dalili nzuri wakati wakijaribu kufika katika fainali yao ya kwanza ya kombe hilo tangu mwaka 1993.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ape / afpe / dpae / rtre
Mhariri: Josephat Charo