Michuano ya CHAN yaanza Morocco | Michezo | DW | 15.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michuano ya CHAN yaanza Morocco

Michuano  ya  kombe  la  mataifa  ya  Afrika  kwa  wachezaji  wa  ligi za  ndani  CHAN  yapamba moto  nchini  Morocco

Kongo Vodoo im Fussball (Getty Images/AFP/I. Sanogo)

Shabiki katika michuano ya bara la Afrika

Katika  michuano  ya  kuwania  ubingwa  wa  bara  la  Afrika  kwa  wachezaji  wanaocheza  katika  ligi  za  ndani ,Namibia  ilipata  bao  la  dakika  za  mwisho  jana  na  kuiangusha Cote d'Ivoire  kwa  bao 1-0  katika  mchezo  wa  kundi B wakati  wa michezo  wa  ufunguzi . Michuano  hiyo  inaingia  katika  mwaka  wa nne  tangu  kuanzishwa  katika  mashindano  ya  ubingwa  wa  bara  la Afrika  kwa   wachezaji  wanaocheza  ligi  za  ndani.

Namibia  na Zambia  zinashikilia  nafasi  ya  juu  katika  kundi  hilo  la B baada  ya Zambia  kuishinda  Uganda  kwa  mabao 3-1.

Sudan iliishinda  Guinea  kwa  mabao 2-1  katika  kundi  A . Leo Jumatatu (15.01.2018) kundi C  linaanza  michezo  yake  katika  mji  wa  kaskazini  wa Tangier,  wakati  mabingwa  wa  mwaka  2014  Libya  ikikumbana  na Equatorial  Guinea  timu  ambayo  ni  ngeni  katika  fainali  hizo wakati  Nigeria  itaumana  na  Rwanda.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo  / afpe / rtre / ape /

Mhariri: Yusuf , Saumu