1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano mikali siku ya mwisho ya Bundesliga

Josephat Charo
25 Juni 2020

Bayern Munich itamaliza msimu wa ligi kuu ya soka Bundesliga ikiwa katika nafasi ya kwanza,na klabu ya Paderbon ikimaliza katika nafasi ya 18. Zimesalia mechi tatu muhimu zitakazochezwa Jumamosi (27.06.2020)

https://p.dw.com/p/3eJqL
Fußball Bundesliga Bayern München - Borussia Dortmund
Picha: Imago Images/Sven Simon/F. Hoermann

Borussia Moenchengladbach na Bayer Leverkusen zimejiimarisha katika nafasi ya nne na ya tano, huku timu zinazomaliza msimu katika nafasi za juu zikijishindia mamilioni ya yuro kutoka ligi ya mabingwa Ulaya.

RB Leipzing, ikishikilia nafasi ya tatu bado haijajihakikishia kuilinda nafasi hiyo kutokana na ushindani ulivyo, lakini tofauti ya mabao matatu na faida ya pointi tatu hakika itawafanya kumaliza ligi wakiwa katika tano bora.

Vilabu vya Wolfsburg na Hoffenheim vyote kwa pamoja vimekwishajihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya kombe la Ulaya msimu ujao zikiwa katika nafasi ya sita na saba katika msimamo wa ligi kuu ya soka ya Bundesliga inayoelekea ukingoni hivi sasa.

Vilabu hivyo vinatofautiana tu kwa magoli lakini nafasi ya juu ina mapumziko ya muda mrefu katika kipindi cha majira ya joto na timu zilizoko chini zinatakiwa kupambana ili kuweza kufaulu.

Klabu ya Paderbon tayari imekwishashuka daraja na Werder Bremen na Fortuna Dusseldorf bado zinakabiliwa na uwezekano wa kuifuata huko, au bahati ya kunusurika na kusalia katika ligi kuu.

Mnyukano utakuwa mkubwa katika kuwania nafasi ya kufuzu kwa ligi ya mabingwa barani Ulaya, Champions, msimu ujao. Borussia Moenchenladbach iliyoko katika nafasi ya nne ikiwa na alama 62 na tofauti ya magoli 25 itafuzu kucheza ligi ya mabingwa endapo watashinda nyumbani dhidi ya Hertha Berlin. 

Bayern Leverkusen yenye alama 60 na tofauti ya magoli 16 itafaulu kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya kama itashinda mchezo wake dhidi ya Mainz na Gladbach ipoteze mechi yake dhidi ya Hertha.

(dpa)