Michezo | Michezo | DW | 20.10.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo

England kuchuana na Afrika kusini katika fainali ya kombe la dunia la Rugby mjini Paris leo na jee Bayern Munich itajiimarisha kilele.wakati ligi kuu ya Ujerumani ikirudi tena uwanjani ?

Mzee Neklson Mandela ambaye ameitakia ushindi timu ya taifa ya mchezo wa Rugby ya Afrika kusini-Springboks leo.

Mzee Neklson Mandela ambaye ameitakia ushindi timu ya taifa ya mchezo wa Rugby ya Afrika kusini-Springboks leo.

Leo ni leo asiye na mwana aeleke Jiwe na asiye na mguu atiye Gongo. Ni fainali ya kombe la dunia la mchezo huo wa Rugby kati ya Afrika kusini na mabingwa watetezi England. Utakumbuka England iliibwaga mwenyeji Ufaransa katika nusu fainali na Afrika kusini maarufu kwa jina la Springboks wakaibwaga Argentina.

Miongoni mwa wachwezaji wanaotegemewa leo katika safu ya England ni pamoja na Phil Vickery ambaye alikuwemo katika kikosi kilichoshinda kombe lililopita la dunia na sasa ni nahodha wa timu hiyo ya England. Katika fainali ya leo katika uwanja wa Stade de Farance anatarajiawa kumuangalia zaidi Os du Randt wa Afrika kusini mchezaji pekee katika timu ya Afrika kusini ilioshinda kombe hilo la Webb Ellis 1995 ilipopambana na England ambayo nayo ililinayakua 2003.

Fainali hii mjini Paris itafanyika kukiwa na matatizo aya kuweaza kufika katika mji mkuu huo wa Ufaransa kwa abaadhi ya mashabiki wa Rugby wa Uingereza kwa sababu ya mgomo wa wafanyakazi wa reli nchini Ufaranasa wakipinga mpango wa Rais sarkozy wa kuondoa utaratibu wa wafanyakazi wa sekta hiyo kustaafu mapema, jambo ambalo limekuwepo kwa kipindi kirefu.

Wakati huo huo shabiki wa michezo , rais mstaafu wa Afrika kusini Nelson mandela, hatohudhuria pambano hilo, kama ilivyotarajiwa awali kwa sababu anahitaji mapumziko baada ya safari nyingi hivi karibuni. Pamoja na hayo Mzee Mandela amezungumza na kikosi cha Springboks kwa njia ya mawasiliano ya Video kuwapa moyo na kuwaambia „ Tunataka vijana wetu muwe na uwezo , nguvu ana moyo wa ushindi kwa mara nyengine kwa sababu sisi na taifa la ushindi.“ Akiongeaza“sina shaka yoyote Springboks itashinda tena kombe hilo na kuja nalo nyumbani.“

Swali wanalojiuliza mashabiki wa mchezo wa Rugby ni jee nani atatamba leo kati ya England na Afrika kusini ? England itarudi na kombe mjini London au litaelekea kusini mwa Afrika mjini Johannesburg.

Katika viwanja vya kandanda ligi kuu ya Ujerumani inarudi tena leo baada ya kusimama mwishoni mwa juma lililopita kutokana na michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya. Miamba ya soka nchini Bayern Munich inakaribishwa na Bochum ilioko katika nafasi ya 14 akiwa na pointi 9. Bayern inaongoza ligi hiyo inayozishirikisha timu 18 ikiwa na pointi 23, mbele ya Karlsruhe na Bremen. Karlruhe inamenyana na Bielefeld.

Mabingwa watetezi Stuttgart wanakaribishwa na Hamburg. Wakati Hamburg yenye pinti 17 iko nafasi ya nne Stuttgart iko nafasi ya 12 ikiwa na pointi 10 . Mkiani ni Cottbus, ikitanguliwa na Duisburg na Nurenbeg na zote tatu zinakabiliwa na hatari ya kushuka daraja.

Matokeo ya michezo hiyo aya ligi pamoja na mengi mengineyo mwishoni mwa Juma ikiwemo fainali ya leo ya kombe la dunia la Rugby kati ya Afrika kusini na England yatakujia katika kipindi chezo cha michezo Jumatatu jioni.

 • Tarehe 20.10.2007
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C7nH
 • Tarehe 20.10.2007
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/C7nH
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com