Michezo wiki hii | Michezo | DW | 05.06.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo wiki hii

Kinyanganyiro cha kufuzu kwa Kombe la dunia 2010

Harambee Stars-Kenya,iliondoka Nairobi kwa mpambano wa kesho na Nigeria huko Abuja, bila kocha wake mjerumani Antoine Hey-Kocha wa simba wa nyika-Kamerun, mjerumani Otto Pfister, nae ameiachamkono Kamerun-kisa nini ?Maandalio ya Kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini yakisonga mbele ,nyoka nao waja mjini kutoka msituni- Je, Kaka wa Brazil atahamia Real Madrid kwa kitita cha dala milioni 92 ? Kinyanganyiro cha kufuzu kwa Kombe la dunia 2010 huko Afrika Kusini, Holland leo (Jumamosi) yaweza kuwa timu ya kwanza ya Ulaya kukata tiketi yake.Kanda ya Amerika Kusini, Brazil imekuwa na miadi leo na Uruguay wakati Argentina ikiongozwa na kocha Maradona ,ilipanga kufuta madhamb ya mabao 6-1 waliochapwa na Bolivia katika mpambano wao na Columbia.

Kaka stadi wa Brazil anaeichezea AC Milan ya Itali, yaonesha amefunguliwa mlango wazi kuiacha mkono klabu hiyo mradi tu kitita cha fedha za kumkomboa kimetimia:Inavuma kuwa kaka anaelekea Real Madrid nchini Spian.Chombo cha habari cha Spian kimearifu kwamba kuhamia Real kwa Kaka kunakaribia.Kima kilichotajwa ni Euro milioni 65 sawa na dala milioni 92.Jumatatu hii ijayo, kaka na waziri mkuu wa Itali anaeimiliki klabu ya AC Milan watakutana kwa chakula cha jioni kupitisha uamuzi juu ya hatima ya Kaka.kikundi cha mashabiki wa AC Milan kiliandamana kati ya wiki nje ya klabu hiyo wakipinga kuhama kwa kaka kutoka AC Milan.

Makocha kadhaa waligonga vichwa vya habari wiki hii.Mbali na kocha wa Taifa wa Harambee Stars-kenya, Antoine Hey kutofuatana na timu yake kwendas Abuja kwa mpambano wa kesho na Nigerioa, kocha wa Simba wa Nyika-Kamerun,mjerumani

Otto Pfister, alijiuzulu.Kisa nini ?

Pfister alikataa kujiunga na kambi ya mazowezi ya simba wa nyika nchini Ubelgiji,baada ya wasaidizi wake aliowachagua kuondolewa na kuteuliwa wapya bila kushauriana nae.Otto Pfister, mwenye umri wa miaka 71 amekuwa kocha wa Kamerun tangu 2007 na aliiongoza hadi finali ya Kombe lililopita la Afrika pale simba wa nyika waliposhindwa kunguruma mbele ya Mafiraouni Misri.

Pfister alichaguliwa kocha wa mwaka wa Afrika 2992 amejikuta akikosolewa tangu pale Kamerun ilipolazwa kwa bao 1:0 na Tojgo Machi iliopita katika kinyanganyiro cha kuania kufuzu kwa Kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini.Simba wa nyika wamepiga kambi Ubelgiji wakijiandaa kwa changamoto ya kesho nyumbani mjini yaounde na simba wa Atlas wa Morocco.Wiki mbili baadae, Kamerun inakutana na Gabon-washindi wa kundi hili A, ndio watakaokwenda Afrika Kusini kwa Kombe la dunia hapo mwakani. Kipa wa zamani wa Kamerun, Thomas Nkono ameshika sasa hatamu kwa muda kama kocha wa simba wa nyika.

Jumapili ijayo, firimbi italia huko Afrika Kusini, kuanzisha Kombe la mashirikisho-Confederations Cup -kombe linalofungua pazia kwa Kombe lijalo la dunia, Juni mwakani: Inaonesha lakini kana kwamba, maandalio ya kombe hilo la dunia pia yanawatoa nyoka pangoni huko Afrika Kusini.Kwani, shughuli za ujenzi wa barabara na kukata misitu, zinawatimua nyoka vichakani na kuingilia majumba ya vitongoji wakisaka usalama na utulivu wao na labda TV za kuangalia kombe la dunia.

Utengezaji wa barabara,viwanja vya ndege na vya mpira unawanyika nyoka maskani zao na wqanapiga hodi majumbani mwa watu.Mnamo miezi 2 iliopita pekee,majoka 24 yalikamatwa na shirika maalumu linalowawinda wanyama kama hao katika eneo la jiji la Johannesberg.hii ni idadi kubwa na isio ya kawaida katika majira ya baridi ambapo nyoka huwa wametulia mapangoni mwao.

Ahmed Nagdee,msemaji wa shirika hilo linalowakoa wanyama wenyed kutambaakee.

Mamlaka ya Reli nchini Tanzania na Zambia -TAZARA, yameandaa treni maalumu itakayowasafirisha mashabiki wa Tanzania wanaotaka kwenda Afrika Kusini kwa Kombe lijalo la dunia:

Naibu mkurugennzi-mtendaji wa Tazara, Damas Nduzmbaro, ameiambia DW kuwa gari-hilo moshi litaanzia safari yake mjini Dar na kupitia Zambia,Zimbabwe hadi kuwasili Afruika Kusini: safari itakuwa Juni mwakani na gari hilo litakuwa na vyumba vya kuishi hadi mwisho wa Kombe la dunia litakaporudi Dar-es-salaam. Abiria na watalii wa Kombe la dunia wanaotaka kujiunga na safari hiyo watakiwa kujiandikisha.

Mwandishi:Ramadhan Ali /RTRE/AFP/DPAE

Mhariri: M. Abdul-Rahman