Michezo wiki hii | Michezo | DW | 13.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo wiki hii

Uwanja wa Taifa kufunguliwa Dar-es-salaam na rais Hu Jintao

Ze Roberto wa B.Munich

Ze Roberto wa B.Munich

Enzi za kustawi kwa mapato ya fedha kwa klabu za Ujerumani za Bundesliga zimeisha kufuatia msukosuko wa uchumi-

FC Barcelona ndio timu maarufu mno barani Ulaya,lakini klabu za Uingereza zimezipiku zile za Spian kuwa na mashabiki wengi-uchunguzi wa hivi punde umeonesha.

Real Madrid ya Spain, ndio klabu tajiri kabisa duniani .

Rais Hu Jintao wa China akiwa pembezoni na rais jakaya Kikwete,mwenyeji wake anatazamiwa kesho(Jumapili) kukata utambi kuufungua rasmi Uwanja wa Taifa,mjini Dar-es-salaam,uliojengwa kwa msaada wa China.Ngoma za burdani na Bongo Flaver zitatumbuiza-aarifu muandishi wetu.

Bundesliga ilirududi jana jioni uwanjani kwa changamoto kati ya viongozi wa Ligi Hoffenheim na Bayer Leverkusen.Macho ya mashabiki lakini yakodolewa changamoto ya jioni hii kati ya Hertha Berlin iliopo nafasi ya 3 ya ngazi ya Bundesliga na mabingwa Bayern munich ambao wako nafasi ya pili wakipania kunyakua leo usukani .

Hadi sasa ni Hamburg iliothubutu kutamba mbele ya Munich ilipoitoa kwa bao 1.mwishoni mwa wiki iliopita,Borussia Dortmund ilijiaribu kuiigiza ilipotangulia kwa bao la kwanza dakika 2 baada ya kuanza mchezo.Lakini, wapi,Munich iliwaambia wadortmund kutangulia si kufika.Mabao 2 ya dakika za mwisho ya miroslav klose baada ya kusawazisha Ze Roberto,yalitosha kuikomoa Dortmund.Berlin,itajifunza jioni hii darasa hilo.

Hamburg inayonyatia kutoka nafasi ya 4 inarudi kesho Jumapili uwanjani ikipambana na jirani zao wa kaskazini Armnia Bielefeld.Hamburg itajaribu kufuta madhambi ya mwishoni mwa wiki iliopita ilipozabwa mabao 3-2 na Karlsruhe ambayo wakati huun iko uwanjani ikicheza na FC Cologne.

Schalke ikijaribu kurudi kileleni ina miadi pia wakati huu na jirani zao Bochum.Mapambano mengine ya Bundesliga ni kati ya Franklfurt na wolfsburg,Bremen na Borussia Moenchengladbach ,kabla kesho jumapili Borussia Dortmund kuonana na Energie Cottbus.

Katika Premier League-Ligi ya Uingereza,kwa kadiri kubwa leo imepumzika ikitoa nafasi kwa kombe la chama cha dimba cha Uingereza FA Cup:

Mabingwa wa Ligi Manchester united wanaania tkketi ya robo finali ya kombe hili kati yao na Derby County baada ya jogoo lao Ryan Gigs juzi kurefusha mkataba kwa mwaka mmoja.

Macho ya mashabiki wa dimba Uingereza lakini yanakodolewa mpambano kati ya Chelsea na Watford.kisa nini ?

Chelsea itakuwa leo na kocha mpya ubavuni baada ya kumtimua mwishoni mwa wiki iliopita kocha wake mbrazil Luis scolari. Kocha mpya ni mholanzi -kocha wa timu ya Taifa ya Urusi -Guus Hiddink.Yeyxe ameahidi kwamba, Chelsea inaweza bado ikatamba msimu huu.

La Liga imerudi uwanjani huko Spain, huku viongozi wa Ligi FC Barcelona wakitamba na jogoo lao la kamerun -Samuel Eto-o,wanataka leo kuigiza rekodi ya mahasimu wao Real Madrid ya kutia jumla ya mabao 107 msimu mmoja. Barcelona inataka kuivunja rekodi hiyo ya mwaka 1989/90.Mahasimu wao leo ni Real Betis ambayo imekuwa ikizotoa jasho klabu nyingi za Spain -msimu huu.

Nje ya Ligi, klabu ya FC Barcelona ya Spain imebakia ndio klabu inayopendwa mno na mashabiki wa dimba barani Ulaya,laklini klabu za Uingereza ndizo zenye mashabiki wengi .

Katika Bundesliga,enzi za klabu kuzidi kutia fedha nono tangu kwa ada za juu hata kupitia matangazo ya biashara na wafadhili yaonesha imemalizika kwa sasa:

"Kabumbu lapasa kutambua wanabiashara hawatazamii kukua kwa uchumi wao."-alisema Peter peters,makamo-rais wa DFL-shirika linalosimamia Bundesliga-ligi ya Ujerumani wiki hii.Zile timu za bundesliga ambazo hazikufunga mikataba ya muda mrefu na wahisani au na washirika wao muhimu wa kibiashara kabla msukosuko wa sasa wa uchumi kuingia,ndizo zenye wasi wasi mkubwa kwa siku zinazotukabili.Kwani, hivi sasa ni taabu kumpata mfadhili anaefaa anaungama Ralf Koenings,rais wa Borussia Moenchengladbach inayoburura mkia wa Ligi wakati huu.

Mkataba wa Borussia na kampuni la zana za uchapishaji la kijapani Kyocera unamalizika mwishoni mwa msimu huu na halijui mambo yatakavyokuwa baadae.

Na Borussia haiko pekee yake katika hali hii.Kuna pia karlsruhe,Energie Cottbus,Bochum na Hertha Berlin-klabu zote hizo zitapaswa kujipatia wafadhili wapya au kufunga mikataba mipya kwa masharti mapya. Wakati timu kama hamburg na Dortmund zinaweza kutoingiwa na wasi wasi zikijua zimesharefusha mikataba yao muda mrefu ujao,klabu hizo 5 ambazo bado hazikufanya hivyo zinakabiliwa na mwaka wa wasi wasi.

Hatahivyo, rais wa schalke Josef Schnusenberg anaamini Bundesliga itaibuka kutoka msukosuko huu wa uchumi imara zaidi kuliko ilipoingia.

Klabu inayoongoza Ligi ya Spain wakati huu FC Barcelona ndio klabu inayopendwa sanya na mashabiki wa dimba barani Ulaya.Uchunguzi umeona mashabiki milioni 44.2 wanaifurahia wakifuatwa na wale wa Real Madrid milioni 41 na nafasi ya tatu inaangukia Manchester U nited kwa mashabiki milioni 37.6.

Katika kundi la klabu 20 bora za Ulaya, klabu za Uingereza sasa zimezipiku zile za Spain kwa muujibu wa uchunguzi huo.Jumla ya mashabiki milioni 114.1 wanapendezewa zaidi na Premier League-ligi ya Uingereza wakati milioni 93.4 tu wanashangiria La Liga-Ligi ya Spain.

Sport U.markt-shirika la michezo na soko mjini Cologne, Ujerumani, limegundua kwamba idadi ya mashabiki wa dimba wa kike wa klabu hizo 20 pia inaongezeka . Galatasaray Istanbul ya Uturuki, ndio inayoongoza upande wa wanawake kwa kiwango cha 54.2 % ikifuatwa na AC Milan ya Itali yenye 50%.

Ukija upande wa klabu tajiri kabisa duniani, taji linakwenda kwa mabingwa wa Spain,Real Madrid,wakifuatwa tu na Manchester united ya Uingereza na baadae FC Barcelona. Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamerejea nao miongoni mwa klabu 5 bora-(top 5) kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 5 na sasa wako nafasi ya 4 huku Chelsea ikiongozwa na tajiri wake mrusi Roman Abramovic ikichukua nafasi ya 5.