Michezo wiki hii | Michezo | DW | 12.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo wiki hii

B.Munich au Hoffehei m kileleni mwa Bundesliga ? Na je, Real itatamba nyumbani mbele ya Barcelona ?

Luca Toni-jogoo la B.Munich

Luca Toni-jogoo la B.Munich

Waandazi wa kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini,wadai wamewanyamazisha wale waliopanga plan B kuandaa kombe la dunia nje ya Afrika kusini- katika La Liga-ligi ya Spian, mabingwa Real Madrid wana nafasi yao ya mwisho jumamosi hii kuhuyisha matumaini ya ubingwa wakikutana na mahasimu wao FC Barcelona. Katika Bundesliga-Bayern Munich waingia uwanjani jumamosi wakimenyana na Stuttgart kuamua ni waoau Hoffenheim kesho,watatawazwa mabingwa wa duru ya kwanza ya msimu. Je,Poland ina uwezo wa kuandaa hata pekee kombe lijalo la Ulaya 2012 ikiwa Ukraine haitamudu.

Bao maridadi la kipindi cha pili alilotia Muivory Coast,Didier Drogba liliisaidia Chelsea kati ya wiki kukata tiketi yao ya duru ijayo ya kutoana ya Champions League-kombe la ulaya.Chelsea ilitoa CDR Cluj ya Romania kwa mabao 2-1.Licha ya ushindi huo,Chelsea iliocheza finali ya kombe hili mwaka jana, imemaliza nafasi ya pili nyuma ya Roma ya Itali ilionyakua nafasi ya kwanza kwa kuichapa Bordeaux.

Panathniakos ya ugiriki waliwasangaza mashabiki wao walipoibuka kileleni mwa kundi B kwsa kuilaza Famagusta ya Cyprus bao 1-0.

Inter Milan kama mlivyosikia ilibidi kuridhika na nafasi ya pili katika kundi hili kufuatia kushimndwa na Werder Bremen ya Ujerumani kwa mabao 2-1.

liverpool iko kileleni na imeingia duru ijayo ya timu 16 kufuatia mabao ya Ryan babel,Albert Riera na david N-Gog kuipatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Eindhoven ya Holland.

Athletico Madrid ,imemaliza wapili katika kundi D baada ya kumudu suluhu 0:0 na Marseille.

FC Barcelona ambayo ilikwisha kata tiketi yake ya duru ijayo, ililazwa kwa mabao 3-2 na Donetsk wakati Sporting Lisbon iliokwishaingia duru ijayo ilitamba kwa bao 1-0 mbele ya Basel ya Uswisi.

Wakati Poland na Ukraine zinajiandaa kwa Kombe lijalo la Ulaya, 2012 , Afrika Kusini inasema haina wasi wasi kombe la kwanza la dunia barani Afrika litachezwa kwao.Ile plan B ilioeleza uwezekano wa kombe hilo kuhamishiwa nchi nyengine sasa imezikwa-wadai waandazi. Eric ponda anasimulia:

"Mpango B" umekufa-alisema Danny Jordaan, mwenyekiti wa Kamati ya Maandalio huko Johannesberg wakati akitoa ripoti ya ukaguzi wake wa mwisho wa mwaka.

Jordaan akizungumzia hapo uvumi ulioenea mapema mwaka huu kuwa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni lilikuwa na mpango B endapo afrika kusini ingeshindwa kuandaa mashindano makubwa kama haya.Hivi sasa, wale waliokua na shaka shaka,na hasa huku Ulaya ,wameambiwa mlikosea.

Hatahivyo, Bw.Jordaan aliarifu ujenzi wa viwanja hivi sasa umeshapindukia dala milioni 315 kuliko ilivyopangwa katika bajeti.Serikali ya Afrika kusini imechangia kitita zaidi cha Rand bilioni 1.4 kusaidia na kuiwachia miji inayochezewa mechi za kombe la dunia nayo kuchangia Rand bilioni 1.8 zilizosalia.

Kombe la mashirikisho linalofungua pazia la kombe la dunia-miaka 2 kabla, litachezwa mwakani kati ya juni 14-28 na litaonesha jinsi Afrika Kusini ilivyojiandaa kwa kombe la kwanza barani Afrika.

Tiketi za kombe hilo la mataifa 8 pamoja na wenyeji,zilianza kuuzwa tangu mwezi uliopita.Mpambano kati ya mabingwa mara kadhaa wa dunia-Brazil na mabingwa wa sasa wa dunia-Itali ndio iliowavutia wengi kununua tiketi hadi sasa.

KOMBE LIJALO LA ULAYA NCHINI POLAND TU ?

Poland inaweza kuandaa kombe la ulaya la mataifa pekee hapo 2012 ikiwa mwenzake Ukraine,haitakamilisha maandalio yake na mapema-alinukuliwa jana kusema Michel Platini, Rais wa UEFA-shirikisho la dimba la ulaya.

Ni mara ya kwanza kwa Platini kuungama uwezekano wa kuipokonya Ukrain haki ya kuandaa ubia kombe la ulaya na Poland.Platini ameelezea shaka shaka iwapo nchi nyengine ingeweza kuchukua nafasi ya Ukraine.ila zimezagaa kuikosoa Ukraine kwamba maandalio yake yamechukua mwendo wa konokono. Je, Ujerumani ibebe jukumu hilo ? "Ujerumani itajitwika jukumu hilo ikiwa bado ujenzi ungali ukiendelea mjini Warsaw ifikapo Juni, 2012. Lakini natia shaka." Platini aliliambia gazeti la Dziennik la Poland.

Serikali ya Ukraine, mwezi uliopita ililivunja shirika la kiserikali lilikuwa na dhamana ya kuandaa kombe la ulaya .hii ilifuatia onyo kutoka UEFA kuwa mambo hayaendi chapchap.

Poland na Ukraine zilichaguliwa bila ya kutazamiwa kuandaa kwa pamoja kombe hilo hapo April,mwaka jana.Zote mbili zimekuwa zikikosolewa kuwa ujenzi hauendi haraka.

Oktoba mwaka huu, Ukraine ilionywa na rais huyo wa UEFA,mfaransa Michel Platini, kuwa itaweza kupoteza nafasi hiyo ikiwa maandalio hadi 2012 hayakufikia daraja inayotakiwa.