Michezo wiki hii | Michezo | DW | 21.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo wiki hii

Kombe la klabu bingwa uwanujani leo

Kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa barani afrika na Kombe la shirikisho kimerudi uwanjani jioni hii huku mabingwa Etoile du sahel wakiumana na As Doune ya Senegal huku mabingwa mara 5 wa kombe hilo Zamalek wamewakaribisha nyumbani Cairo -Asec Abidjan ya Ivory Coast.

Simba ya Tanzania imekwenda Nigeria kwa miadi na Enyimba wakati katika kombe la shirikisho Young Africans -mahasimu wao nyumbani walifunga safari ya Libya.

Wakati bayern munich ilikata tiketi yake ya finali ya kombe la shirikisho la dimba la Ujerumani ,imekuwa hivi punde uwanjuani na Leverkusen ,duru ya mwishoni mwa wiki hii ya Bundesliga inakamilishwa na mapambano 2 kesho kati ya Bremen na Bielefeld wakati schalke inaitembelea Hertha Berlin hapo kesho.

Katika medani ya riadha ,majogoo wa kenya wanajiwinda kwa mbio za nyika za ubingwa wa dunia huko Scotland baadae mwezi huu .

►◄

Kinyan'ganyiro cha vikombe 2 vya Afrika kimerudi uwanjuani mwishoni mwa wiki hii huku simba ya Tanzania ikiitembelea Enyimba huko Nigeria katika zahama za klabu bingwa.Wenzao Yanga walifunga safari ya Libya katika changamoto za Confederations Cup-kombe la shirikisho la dimba la Afrika (CAF).

Kabla kuondoka Dar-es-salaam kwa safari ya Nigeria ,simba walituma salamu kwa Enyimba kwamba hwakusudii kurudi Dar-es-salaam mikono mitupu.

Mabingwa wa kombe hili Etoile du sahel ya Tunisia,walikuwa na mteremko nyumbani leo kwani wakicheza na AS Doune ya Senegal wakati mabingwa mara 5 Zamalek wamekuwa na miadi nyumbani cairo na ASECAbidjan ya Corte d'Iviore.ASEC ilikusudia msimu huu kutamba na kutoaga na mapema kama msimu ujao kinyan'ganyiro hiki.ASEC ni timu ya 3 tu ya Afrika kuwahi kutetea taji lao.

Mabingwa Etoile du sahel, walikuwa na wasi wasi wa kutocheza jogoo lao lililotia mabao 8 msimu uliopita na kupelekea kutawazwa mabingwa Amine Chermiti.

Katika kinyan'ganyiro cha pili,Young Africans ya Tanzania imekwenda Libya kutimiza miadi yake ilioweka na Al Akhdar.

Mashabiki nyumbani Tanzania wakisubiri kwa hamu kujua ni nani kati ya simba na yanga hareejei mzizima mikono mitupu.

Kati ya wiki hii kinyan'ganyiro cha kuania tiketi za dimba la olimpik huko Beijing,China kiliendelea baada ya wiki iliotangulia kiasi cha wachezaji 7 wa timu ya taifa ya Kuba kuiachamkono timu yao na kutoroka.

Marekani iliocheza wiki iliopita na Kuba pamoja na hondurus zimekata kwahivyo tiketi zao za dimba la olimpik baada ya ushindi wao juzi alhamisi.Freddy Adu,muamerika wa asili ya Ghana aliufumania mara mbili mlango wa kanada na kukamilisha ushindi wa mabao 3-0 huko Nashville wakati hondurus iliilaza Guatamala mabao 6-5 kupitia Kati ya wiki hiichangamoto za mikwaju ya penalty .

Changamoto za Bundesliga zitarudi uwanujani kesho kwa mapambano 2 yanayokamilisha duru ya leo ambayo ilizikumbanisha timu 2 za kileleni na ambazo zimeingia nsu-finali ya kombe la shirikisho la dimba la ulaya (UEFA)-Bayern Munich inayoongoza Ligi na Bayer Leverkusen.

Kesho jumapili, Bremen inacheza na Bielefeld wakati Schalke inaitembelea Hertha berlin huko mji mkuu.

Ligi ya Uingereza-premier League kesho ni asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo mkutano uwanjani-Chelsea inacheza na Arsenal wakati manchester United inaumana na Liverpool.Hayo ni mapambano 2 ya kukata na shoka.

Ama katika La Liga-Ligi ya Spain FC barcelona ambamo mkamerun Samuel Eto'o amerudi kutamba kinyume na Ronaldinho, wanacheza nyumbani na Real Valladolid wakati mahasimu wao Real madrid wananyan'ganyia pointi 3 kati yao na Valencia.

Huko Holland macho yanakodolewa changamoto ya kesho kati ya Enschede na Ajax Amsterdam na Sparta Rotterdam dhidi ya Feynoord Rotterdam.

Wafaransa wao wanajinoa makucha kuona mpambano wa kesho kati ya Olympique Lyon na Paris St.Germain na Stade Rennes na Racing Lens.

Kati ya wiki ijayo,duru ya kuania tiketi za kombe lijalo la dunia 2010 huko Afrika kusini kwa kanda ya Asia ,itaanza kwa kishindo:Halkadhalika , timu kadhaa za taifa zitakuwa uwanjani kupimana nguvu kwa dimba la kirafiki:

Brazil itakuwa mjini London kwa changamoto na Sweden katika marudio ya finali ya 1958 pale Pele alipoichezea mara ya kwanza Brazil katika kombe la dunia.

Ujerumani itakwenda Uswisi kuujaribu uwanja wa huko kwa kinyan'ganyiro cha Juni hii cha kombe la Ulaya la mataifa.

Mjini Dusseldorf, Ujerumani, mashabiki watajionea mpambano wa kusisimua kati ya Ureno na Ugiriki-marudio ya finali ya kombe lililopita la Ulaya,iliomalizika kwa ushindi wa wagiriki.

Ni nafasi nyengine hiyo ya kumuona Christiano Ronaldo.Ufaransa itaikaribisha Uingereza mjini Paris wakati mabingwa wa dunia-Itali wataumana na Spian.Russia inakamilisha kalenda ya jumatano hjii na Romania .

Ama katika kinyan'ganyiro cha kuania tiketi za kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini,kanda ya Asia,Qatar inacheza na mabingwa wa Asia-Iraq huku china wana miadi na Australia.Oman inaitembelea Thailand wakati bahrein inatamba nyumbani mbele ya Japan.Ndugu 2 Korea ya kusini wanakutana na korea ya kaskazini mjini Shanghai,China wakati Uzbekistan inachuana na Saudi Arabia.Kuweit itaikaribisha Iran.

Kati ya wiki hii ilikua zamu ya kinyan'ganyiro cha kombe la shirikisho la dimba tangu Spain hata Ujerumani:

Bayern munich kama mahasimu wao wa duru ijayo ya kombe la UEFA FC Getafe ya Spain zimeingia finali ya kombe hilo.Getafe baada ya kuilaza Racing Santander mabao 3-1 duru ya kwanza ilimudu kati ya wiki hii sare ya bao 1:1 .hii ilitosha kuikatia Getafe tiketi yake ya finali ya kombe la Copa del Rey.

Mahasimu wao katika finali watakuwa FC valencia ilioitoa nje FC Barcelona. Kwahivyo, Bayern munich inabidi kusikia salamu hizo ilizotoa Getafe watakapokumbana katika kombe la ZEFA duru ijayo.

RIADHA:

Bingwa wa zamani wa pentahlon wa marekani Joyner-Kersee amesema bingwa wa sasa wa Olimpik mswede

Carolina Kluft akishiriki au asishiriki katika mashindano 7 mbali mbali -heptathlon katika michezo ijayo ya olimpik, tayari yeye ana hadhi ya juu kabisa ya wakati wote.

Jackie ndie bingwa wa rekodi ya dunia katika heptathlon.

Kushinda mara 3 ubingwa wa dunia,mara moja medali ya dhahabu ya Olimpik na mara mbili kukusanya hadi pointi 7000 kumemuweka maisha kileleni Carolina Kluft.

Macho ya wanariadha wa mbio za nyika-world cross country championship yanakodolewa huko sctoland wakati huu.wanariadha hasa wa Kenya na Ethiopia wamo kujinoa wakati huu kwa kinyan'ganyiro hicho.Licha ya machafuko ya wiki chache zilizopita nchini Kenya, wanariadha wake kwa waume wanasema sasa wako tayari kurudi Kenya na medali huku wakiendelea na mazowezi na kujinoa kwa mashindano ya mbio za nyika huko Scotland .

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com