Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 15.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Bayer Leverkusen yarudi kutamba Bundesliga

Bayer Leverkusen

Bayer Leverkusen

Katika Bundesliga, Stefan Kiessling sio tu anaongoza orodha ya watiaji mabao mengi katika Bundesliga, bali pia aliirudisha jana Bayer Leverkusen kileleni hadi pointi 1 tu nyuma ya viongozi wa Ligi, Bayer Lverkusen.

Katika Premier League, Muivory Coast, Didier Drogba, aipelekea salamu Ligi ya Uingereza kuwa klabu yake, Chelsea, mwishoe itatamba .Guus Hiddink, akataa kuwa kocha wa Ivory Coast katika Kombe lijalo la dunia.Simba yanguruma na kuvaa taji na mapema katika Ligi ya Tanzania.

Bayer Leverkusen imeikomea Hamburg jana mabao 4-2 na kurejea kuwa na usemi wapi Kombe hili msimu huu linaelekea. Katika kinyan'ganyiro cha timu 3 cha kuania taji la ubingwa, Munich, Schalke na Bayer Leverkusen, Bayer Leverkusen jana ilifufuka kutoka pigo la kushindwa mara ya kwanza tangu mapambano 25 mwishoni mwa wiki iliotangulia huko Nürmberg na kumtuliza shetani wake kutwaa pointi 3 mjini Hamburg. Kiessling, alilifumania lango la Hamburg mara 2 hapo jana. Hamburg, ilipigana kuzima hujuma za wageni wao, lakini, mwishoe, walikuja hadi mabao 2-3 kabla ya Leverkusen kuwaangusha kabisa kwa maba0 4-2.

Bayern Munich,Ijumamosi, iliitimua nje Freiburg, kwa kuichapa mabao 2:1 pale mdachi Arjen Robben, alipopiga hodi mara 2 katika lango la Freiburg na kukaribishwa mikono miwili.Kocha wa Bayern Munich, inayoongoza sasa Bundesliga kwa pointi 1, huku Leverkusen ikiifukuzia nyuma, Van gaal alisema,

"Kuwa mwishoe, tulishinda ni uzuri, lakini ingeweza pia mchezo kuishia hata sare bao 1:1 au 1:0."

Nae kocha wa Bayer Leverkusen, Jupp Hynckes, baada ya kuifedhehe Hamburg kwa mabao 4:2 alisema,

"Mara tu ya kipindi cha mapumziko nilin'gamua kuwa wachezaji wangu wameelewa mambo yalivyo, na hapo wakaanza kusaka mbinu ya ushindi na kutia mabao maridadi kabisa."

Mdachi Guus Hiddink, alietazamiwa kuwa kocha mpya wa Ivory Coast na kuiongoza katika Kombe lijalo la dunia Juni hii nchini Afrika Kusini, ameamua kutoiacha mkono Urusi. Hiddink alisema na ninamnukulu:

"Yapasa niungame kwamba Ivory Coast haikuufanya uamzi wangu kuwa rahisi. Kwani Didier Drogba alinipigania sana niwe kocha wao na hata Rais wa Shirikisho la dimba la I.Coast, Jacques Anouma." Hiddink alisema amelazimika kumaliza mkataba wake na Urusi.

Simba imenguruma tena nchini Tanzania na kwa mara ya kwanza tangu kususiwa klabu hii 1936, imeshinda mapambano 20 mfululizo. TSimba iliikomea Azam mabao 2:0 na kutoroka na taji na mapema.

Mwandishi: Ramadhan Ali/ AFPE

Uhariri: Miraji Othman