Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 16.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Ujerumani inamenyana na Austria leo kuania tiketi ya robo-finali ya kombe la Ulaya.Tanzania yamudu sare 0:0 na Kamerun.

Nahodha wa Ujerumani M.Ballack

Nahodha wa Ujerumani M.Ballack

Kocha wa Ujerumani inayocheza leo na Austria mjini Vienna, asema aelewa ni timu gani ataiteremsha hivi punde uwanjani:

Taifa Stars-Tanzania yawazuwia simba wanyika-Kamerun kunguruma mjini Dar-es-salaam:

Harambee Stars-Kenya,yaichezesha Zimbabwe kindumbwe-ndumbwe uwanjani Kasarani:

Brazil ilinyolewa jana bila ya maji na Paraguay na kuzabwa mabao 2:0 katika kinya n'ganyiro cha kanda ya Amerika kusini kuania tiketi za kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini.

Tuanze na kinyan'ganyiro cha jioni hii cha kukata na shoka baina ya mabingwa mara 3 wa Ulaya-Ujerumani na Austria:Je, Ujerumani itanyolewa tena na wembe ule ule uliowanyoa Cordoba,Argentina 1978 na kuwapiga kumbo nje ya kombe la dunia ?

Wenyeji Austria wanasaka ushidi mwengine dhidi ya Ujerumani ili kusalia mashindanoni na wanacheza nyumbani.Lakini, je, jogoo la shamba litawika mjini Vienna ? Ujerumani inahitaji sare tu kuifuata Croatia inayiocheza leo na Poland katika duru ijayo ya robo-finali:Austria imepata nguvu baada ya kumudu sare ya bao 1:1 na Poland katika mpambano wake uliopita:Je. Ujerumani au Austria itaaga Kombe la ulaya usiku huu ?

Katika mechi ya pili leo, Poland inaumana na Croatia,lakini Croatia haina uchu leo wa ushindi na yamkini ikateremsha timu B na hivyo kuipa matumaini Poland ya ushindi.

Kinyan'ganyiro cha kuania tiketi za kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini kiliendelea mwishoni mwa wiki tena katika kanda za asia,Afrika na Amerika kusini.

Msangao ulizuka Dar-es-salaam pale Taifa Stars walipowazima simba wa nyika kamerun wasingurume porini mwao.

Huko Amerika kusini, Brazil pia ilizimwa vishindo vyake na Paraguay tena iliocheza na wachezaji 10 tu-kisa nini ?

Paraguay ikicheza na wachezaji 10 tu uwanjani ilistusha jana Brazil ilipoichapa mabao 2:0.Kwa ushindi huo Paraguay imeparamia kileleni mwa kanda ya timu za Amerika kusini kwa kombe la dunia 2010.Argentina ilihitaji bao la dakika za mwisho za kufidia kuepuka kuaibishwa nayo na chipukizi Ecuador.

Mjini Dar-es-salaam, Taifa Stars,walizuwia vishindo vya simba wa nyika na nahodha wao Rigobert song na nani alietazamia hayo ? Mwishoe timu hizo 2 zilitoka suluhu 0:0.duru ijayo itakua Yaounde na simba wa nyika wakiwa pori lao,Taifa Stars watabahatika sana wakirudia matokeo ya jana.

Wakati Taifa Stars ilimudu suluhu nyumbani na simba wa nyika-Kamerun, Harambee Stars walidhihirisha kwamba ule ushindi wao wa mabao 2:0 wiki iliopita dhidi ya Guinea haukua fluke au bahati nasibu walipotamba uwanjani Kasarani mbele ya Zimbabwe.Kenya iliilaza Zimbabwe mabao 2:0.

I

►◄